Kiukweli Tangawizi hutumiwa sana ambapo jamii mbalimbali duniani hutumia kwa matumizi tofauti tofauti ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na pia kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali.
FAIDA ZAKE
KATIKA LISHE;
– Tangawizi ikichemshwa na maji na kuongezwa sukari hutoa kinywaji ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana yaani chai ya tangawizi. – Hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali kama biskuti, mikate, keki, nyama na vingine vingi.
MATIBABU
-Utomvu wa zao hili umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo vya binadamu. Ukichua utomvu huu mara mbili kwa siku sehemu zenye maumivu huweza kuondosha maumivu mbalimbali haraka, kwa mfano maumivu ya misuli, magoti, maumivu ya kichwa nakadhalika.
– Hukinga na kutibu kuwashwa na kukereketwa koo na ugonjwa wa mafua ya sehemu ya juu.
– Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.- Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni. Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.
SUPU YA TANGAWIZI
– Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.- Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.- Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo
– Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.- Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua.
Sasa unasubiri nini kuitumia? Endelea kusoma Simamia.com kesho ntakuletea faida za Tangawizi kwa Mwanaume
@Afya yako
Recent Comments