yes 250

KUWEKA AKIBA YA CHAKULA NI JUKUMU LA KILA MTU

NA,ANKO G

Asilimia kubwa ya watanzani wanategemea kupata chakula baada ya kutoka na kwenda kutafuta chakula kila siku maana yake ili wale lazila watoke na kwenda kutafuta jambo linaloweza kupelekea watu wanapo kutana na changamoto ya kushindwa kutoka kutafuta basi wanaweza shindwa kula.

Utamaduni huu umechuliwa kama unatokana na kipato kidogo lakini hata wenye uwezo wa kuweka akiba ya chakula wamejikuta wakishindwa kuweka akiba kwasababu imeonekana kuwa ni utamaduni wa kawaida wa kununua chakula cha muda mfupi.

Hata hivyo hata wakulima wengi wamejikuta wakikabiliwa na uhaba wa chakula kwasababu wengi wamekua na utamaduni wa kuuza mazao wanayo vuna na kusahau kuweka akiba jambo linalo pelekea kukosa chakula na kuanza kununua chakula kama ilivyo kwa watu ambao siyi wakulima.

Vilevile hali ya kushindwa kuweka akiba ya chakula inapelekea kuwa na matumizi makubwa kwasababu ya kununua chakula kidogokidogo na maranyingi chakula kinatabia ya kupanda bei kutokana na msimu na kuadimika kwa baadhi ya mazao.

Hivyo basi hali hii inaweza kupelekea janga la njaa pale yanapo tokea majanga kama ilivyo tokea kipindi cha ugonjwa wa Uviko – 19 ambapo watu wengi walikua hawawezi kutoka nje na kutafuta pesa ama kutafuta chakula.

Lakini pia hali hii inaweza kupelekea janga la njaa kama hali iliyopo kwasasa ya mfumko wa bei za bidhaa kutokana na vita inayo endelea Iran ambapo wengi wanaweza shindwa kumudu gharama ya vyakula.

Na wakati mwingine linaweza tokea janga la nja pale linapo weza kujitokeaza janga la ukame au mvua zinazo pita kiasi ambapo majanga hayo yanaweza kuathiri uzalishaji wa mazao ya chakula jambo linalo weza kupelekea ukosefu wa chakula na chakula kupanda bei maradufu.

Kuweka akiba ya chakula ni kuokoa gharama na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya chakula kwasababu kinanunuliwa kwa bei ya jumla na inasaidia pale yanapotokea majanga yanayo athiri utafutaji wa fedha,mfumko wa bei na majanga yanayo athiri uzalishaji wa vyakula.

Kila mtu ajifunze kuweka akiba ya chakula kwasababu ni mhimu katika maisha ya kila mtu na sarikali inatakiwa kuweka mkazo katika kuweka akiba ya chakula kwaajili ya kujilinda pale majanga yanapotokea walau kila wilaya iwe na ghara la serikali la kuhifadhi akiba ya chakula

About Anko G

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Endelea Kupata Habari Mbalimbali, Weka Email Yakol

Habari, Uchambuzi, Burundani na n.k.