CHAMA cha Wasioona Tanzania (TLB) kimelitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka mazingira rafiki kwa watu hao wakati wa Uchaguzi Mkuu 25 Oktoba mwaka huu. Anaandika Faki Sosi ⦠(endelea).
Hatua hiyo imekuja baada ya NEC kutoandaa utaratibu mzuri wakati wa kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa njia ya kielektronik (BVR).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TLB, Luic Benedicto amesema kuwa, BVR imewatia hofu watu wenye ulimavu wa macho kukosa haki yao ya msingi kikatiba ya kupiga kura.
Benedicto amesema, kutokana na kutofautina kwa utaratibu wa kujiandikisha baina ya watu hao wasioona ndiko kumewatia hofu ya kukosa haki ya kupiga kura kwani watu wao wote walitakiwa kutumia saini maalum(RHT) au kusaini kwa dole gumba.
âMimi mwenyewe binafsi nilishangaa kuona msimamizi wa uandikishaji amenisainisha kwa kunishika mkono na kunifuatishia saini yangu hii inanipa mashaka baada ya kusikia wengine wamefanyiwa utaratibu tofautiâ.amaesema benedicto.
Amesema kuwa, kupiga kura ni siri ambayo haina rafiki wala mpenzi wa kumuamini ,kutokana na kuwa wao wanawekewa utaratibu wa kusindikizwa na mtu mwengine ,hivyo wanaitaji kuwekewa utaratibu mwingine wa kuwatambua wagombea wakiwa peke yao.
Nakwamba, NEC ilitakiwa kutoa ufafanuzi mapema kuhusu njia za kuwasaidia walemavu wa macho jinsi ya kumchagua mtu wanayemtaka kuliko kusaidiwa kupiga kura.
Aidha, amesema kuwa chama hicho hakina itikadi yoyote kwani chama chochote cha siasa kwani wanaamimini chama kinaweza kuwa serikali na kuwasaidia.
Amesema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya mwenyekiti wa shirikisho la walemavu Tanzania, Amoni Mpanje alipoonyesha kuwa walemavu wote wanamsapoti mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Magufuli ikiwa chama hicho hakina itikadi ya chama chochote kila mtu anaitikadi zake
âTumesikitishwa na kile alichoongea Bwana Mpanje alipokuwa kwenye kampeni sisi hatumkatazi kuwa na chama lakini sio kusema chama cha walemavu wapo upande Fulani kila mtu anaitikadi yake kwani tusikione chama cha waalimu,madaktali au wakulimakatika kampeni hizo za siasa licha ya kuwa wanaongeza watu wenye itikadi tofuati.â amesema Benedicto
Recent Comments