AKIWA katika maandalizi ya kuanza harakati za kuomba kura kwa wananchi wa Morogoro Mjini anapogombea nafasi ya ubunge mkoani humo, mkali wa hip hop nchini, Seleman Msindi âAfande Seleâ, amejikuta akiwekewa pingamizi lenye madai kwamba hajui kusoma na kuandika.
Afende Sele alisema ameshangazwa na pingamizi hilo lisilo na maana katika siasa kwa kuwa haliwashtui wapigakura wake kwa kuwa wanamfahamu vizuri ngazi zote za shule alizopitia.
âNimeshangazwa nilipoitwa kwa mkurugenzi Manispaa ya Morogoro mjini akaniambia nimewekewa pingamizi na chama kimoja wapo mkoani huko wakidai sijui kusoma na kuandika, sasa huo si upofu wa kisiasa, ninachojua ni kwamba wananiogopa hivyo wanahangaika kuniwekea vizingiti vingi,â alisema Afande Sele.
Aliongeza kwamba, pingamizi hizo hazina faida kwa wananchi wanaotaka wawaongoze kwa kuwa wanamfahamu na ana elimu nzuri inayomwezesha kuishi maisha ya kawaida kama wananchi wengi wa mkoa huo.
âKuchafuana huko kusiko na maana hakujengi mkoa wetu wala hakuwakwepeshi wananchi wa Morogoro mjini kukwepa kupiga kura, watapiga kura na kwa kuwa nina uhakika wananifahamu na wanataka kiongozi aliyekaribu nao na anayejua shida zao, sina shaka na wanaonichafua kwa kuwa hofu yao haitowaisha hadi nitakaposhinda,â alieleza Afande.
Afande ni mmoja wa wasanii watakaogombea ubunge kwa mwaka huu wa 2015 wengine ni Joseph Haule âProfesa Jayâ anayegombea ubunge jimbo la Mikumi (Chadema), Irene Uwoya viti maalumu Tabora (CCM), Kingwendu anayegombea Kisarawe kupitia (CUF), Mohammed Mwikongwe âFrank wa Kaoleâ, anagombea Segerea kupitia (ACT).
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments