SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetangaza uwepo wa vipande vya umemejua visivyo na ubora katika soko la ndani. Shirika hilo limewataka watumiaji wa umemejua kuwa makini wanapoenda kununua vifaa vya kutengeneza mfumo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu matokeo ya uchunguzi wa maabara wa sampuli zaidi ya 10 za vipande hivyo vya umemejua vilivyochukuliwa madukani kuthibitishwa ubora, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma cha TBS, Roida Andusamile alisema, matokeo ya maabara yameonesha sampuli zote zilizopimwa hazina ubora.
Uchunguzi huo ulitokana na malalamiko ya watumiaji wa umemejua pamoja na Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), kuhusu uwepo wa vipande vya umeme jua vilivyo hafifu. âBaada ya kupata malalamiko, maofisa wetu pamoja na TAREA walifanya manunuzi maalumu katika maduka mbalimbali ya vifaa hivyo yaliyopo Kariakoo, kwenye mitaa ya Msimbazi na Congo, pamoja na eneo la Keko-Mwanga, Dar es Salaam kupata sampuli ili kuthibitisha ubora,â alisema Andusamile.
Hata hivyo, alisema wataalamu wa upimaji ubora walibaini kasoro nyingi zinazosababisha vifaa hivyo viwekwe katika kundi la vifaa visivyofaa kuingizwa sokoni. Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora cha shirika hilo, Ashura Kilewela alisema vifaa vilivyopimwa vilinunuliwa kutoka duka la Regal Solar Limited, duka la Keoali Power & Equipments Co. Limited na duka la Nishati Electronics Limited.
âKatika duka la Regal Solar tulizuia vipande 1,321 vya umemejua visiuzwe na kwenye duka la Nishati Electronics tulizuia vipande 164 visiuzwe kwa sababu tulivitilia shaka ya ubora, jambo ambalo sasa limethibitika kuwa ni kweli havifai kwa matumizi,âKilewela alisema.
Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa TAREA, Mathew Matimbwi alitaja baadhi ya kasoro zilizokutwa katika vipande hivyo, ambazo wananchi wanapaswa kuzifahamu kuwa ni seli za vipande hivyo kuwa na rangi mbili badala ya moja na kutoandikwa nchi zinakotoka.
Kasoro nyingine ni kipimo cha nguvu ya umeme inayotoka kuwa ndogo ikilinganishwa na kiwango cha chini cha nguvu ya umeme kinachotakiwa kutoka, lebo ya kampuni inayozitengeneza kubandikwa kwa stika ikionesha inatengenezwa Ujerumani wakati si kweli.
Recent Comments