WAKAZI wa Uyovu wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita wamelalamikia huduma mbovu za afya hususani akina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na wazee. Anaandika Dany Tibason, Bukombe ⦠(endelea).
Wananchi walitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge na madiwani jimbo la Bukombe uliofanyika katika viwanja vya Uyovu.
Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Salum amesema licha ya serikali kudai huduma za afya kwa makundi hayo ni bure lakini imekuwa kinyume.
Mariam amesema kwa sasa katika zahanati nyingi za wilaya ya Bukombe akina mama wamekuwa wakichangishwa michango mbalimbali pamoja na kuuziwa kadi ya kliniki na vifaa vingine.
Kwa upande wake baadhi ya wazee wamesema kuwa serikali imewatelekeza kwa kuwalaghai kuwa wanatakiwa kutibiwa bure lakini wanatozwa hela.
Juma Khamis ambaye ni kati ya wazee wa Bukombe amesema wamefikia hapo walipo kutokana na kuwepo kwa maneno mengi mazuri ya serikali ambayo utendaji wake ni mgumu.
Naye Mgombe Ubunge jimbo la Bukombe, Prof. Kulikoyela Kahigi kwa tiketi ya Chadema, amesema serikali haina nia ya dhati kuwasaidia wananchi.
Kuhusu masuala ya madawa Prof. Kahigi amesema Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inaidai serikali jumla ya Sh. 100 bilioni. âKwa hali hiyo mnadhani serikali ina nia njema na wananchi hata mkidhani Dk. John Magufuli ni mzuri lakini chama chake kimeoza,â amesema.
Kwa upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Uyovu, Yusuph Fungameza (Chadema) amesema sera ya kata na chama kwa ujumla.
Mbali na hilo amesema Chadema inaamini zaidi katika kuwepo kwa amani, hivyo katika kampeni lazima utulivu na amani vilindwe.
Akizungumzia vipaumbele Mgombea Udiwani Kata ya Igulwa, Soud Ntanyagala (Chadema) kipaumbele ni elimu, afya pamoja na maji.
Amesema ni ajabu kwa wale ambao wanasema hakuma maendeleo katika jimbo la Bukombe wakati ndani ya miaka mitano sekta ya elimu imepanda, huduma ya umeme imepatikana na mambo mbalimbali.
Recent Comments