Jenerali Gilbert Diendere aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso amesema kuwa yupo tayari kukabidhi serikali kwa utawala wa kiraia kama ilivyopendekezwa na wapatanishi.
Diendere ambaye alipindua serikali hiyo siku ya alhamisi wiki iliyopita anasema kuwa alifikia uamuzi huo kwa lengo la kile anachokiita kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
Kauli yakekukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou
Jeshi la Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na mapinduzi hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo tu watasalimisha silaha zao.
Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
Mamia ya watu wamezagaa mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kwaajili ya kusherehekea.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments