RAIS Jakaya Kikwete ametaja changamoto zinazosababisha utalii wa Afrika usikue kwa haraka kuwa ni ukosefu wa miundombinu bora ya kitalii, utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.
Alisema, pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, changamoto hizo zinalifanya bara hilo libaki nyuma katika kuvutia watalii wa kimataifa, hivyo kuendelea kuwa na mapato madogo yanayotokana na sekta hiyo.
Aidha, alisema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi, pamoja na kudhibiti ujangili dhidi ya tembo. Alisema, kutokana na jitihada zinazofanywa kuukomesha, katika mwaka uliopita ujandili umepungua.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa shughuli za miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika (ATA) na miaka 10 ya Jukwaa la Rais kuhusu Utalii, kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York jijini New York.
Rais Kikwete aliyeko Marekani kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya jopo la watu mashuhuri duniani wanaotafuta njia inayoweza kutumiwa na dunia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko alisema asilimia 36 ya eneo lote la nchi yake litatengwa kwa ajili ya shughuli za hifadhi.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na Waafrika wenyewe, ili picha inayojengwa kuwa tatizo lililo katika nchi moja ni tatizo la bara zima la Afrika ijulikane kuwa si sahihi.
Alisema, âNi lazima itafutwe nia ya kulisahihisha jambo hilo kwa sababu Afrika ni bara lenye nchi 54 na si nchi moja na majimbo 54â. Kuhusu mapato ya utalii, alisema mwaka jana Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa waliotembelea maeneo mbalimbali duniani na asilimia tano ya watalii wote waliotembelea dunia mwaka jana.â
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alishangiliwa wakati alipowaambia washiriki: âNapenda kuchukua nafasi hii pia kuwaaga marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni ya mwisho kwangu nikiwa Rais wa nchi yangu…â. âNitaondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu nikiwa nimekamilisha vipindi viwili vya uongozi kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.â
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments