SERIKALI imejipanga kumaliza madeni inayodaiwa na walimu kwa awamu, ambapo zaidi ya Sh bilioni 1.7 zitaanza kulipwa kuanzia wiki ijayo na kutekeleza muundo mpya wa utumishi, ambao ni pamoja na kupandisha vyeo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Utumishi, Hab Mkwizu alisema madeni ya mishahara ya kuanzia Desemba 2013 hadi Agosti mwaka huu, yanahusu walimu 60,322 sawa na madai ya Sh bilioni 29.8 yaliyowasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kwa ajili ya uhakiki na tayari halmashauri 103 zimeshahakikiwa.
Alisema uhakiki wa halmashauri zilizobaki unatarajiwa kukanilika Oktoba 11 mwaka huu na fedha zote zitatumwa kwa halmashauri husika mara baada ya uhakiki kukamilika. Kati ya kiasi hicho cha fedha wanazodai walimu, Sh bilioni 21 ni za waalimu shule za msingi ambao ni 44, 715 na Sh bilioni 8.6 wa shule za sekondari ambao ni 15,607.
âWalimu 45,453 wanadai malimbikizo ya mishahara Sh bilioni 32 hadi kufikia Septemba mwaka huu. Serikali ilikuwa imewalipa walimu 3,979 Sh bilioni 2.3 na wengine ambao bado wanadai watalipwa mwezi huu,â alisema Mkwizu.
Alisema madeni ya Sh bilioni 1.73 ya walimu 1,667 ndio yatalipwa mwezi huu huku wengine wakiendelea kulipwa kila mwezi kadiri ya uhakiki unavyokamilika na kwamba madeni yasiyohusu mishahara yamekuwa yakilipwa kupitia fungu la matumizi mengineyo.
Mkwizu akifafanua madeni ya waalimu, alisema Serikali imeagiza pia kila halmashauri kufanya vikao vya kuwapandisha madaraja walimu mapema iwezekanavyo kabla ya Novemba mwaka huu. âWalimu waliokaa kwenye cheo kimoja kwa muda mrefu na wale wanaokaribia kustaafu watapewa kipaumbele katika upandishaji vyeo,â alisema Mkwizu.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments