RAIS wa Namibia, Dk Hage Geingob ameipongeza serikali kwa kubadilishana uongozi kwa amani na utulivu. Amesema hatua hiyo inaonesha ukomavu wa hali ya juu wa demokrasia. Aidha, Geingob amesema ana imani kuwa Tanzania itafanya uchaguzi wake kwa amani.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo muda mfupi, baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili, Geingob aliwataka Watanzania kuendelea kulinda amani iliyopo, ambayo nchini nyingi duniani bado zinahangaika kufanikiwa kuwa nayo.
âLeo Rais (Jakaya) Kikwete umesimama kwa ufahari na kusema unaondoka madarakani baada ya wiki mbili ukiwa na furaha na hauna hofu. Nami najisikia fahari kwa sababu hata rais aliyenitangulia alizungumza kuwa ni muhula wake wa pili na wa mwisho.
â Hii ni hulka ya viongozi wa sasa wa nchi nyingi za Afrika, isipokuwa nchi chache. Ninawaheshimu marais ambao wanakabidhi madaraka kwa amani,â alisema. Geingob alisema ana imani kubwa kuwa Watanzania, watafanya uchaguzi wao kwa amani na utulivu na atakayechaguliwa atakuwa ni chaguo la wananchi.
Alisema Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa muda mrefu, jambo ambalo lilifanya viongozi wa nchi kadhaa, ikiwamo Namibia, kukimbia ubaguzi katika nchi zao na kuja kujifunza na kisha kupigania uhuru wa nchi zao. âTulikimbia kutafuta amani na tulikuja kisiwa cha amani, Dar es Salaam.
Hapa ndipo tulipoishi na kujifunza kupigania haki za binadamu na kukomboa nchi zetu. Ndio maana bado tunaheshimu mchango wa hayati Mwalimu (Julius) Nyerere aliyeiongoza Tanzania. Rais Jayaka Kikwete alimhakikishia mgeni wake kuwa Serikali itahakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
â Nina imani chama changu (CCM) kitashinda kama ilivyoshinda SWAPO.â Akijibu swali kama anaondoka madarakani ameweza kutekeleza malengo aliyojiwekea, Kikwete alisema: â Siyo yote, ila mengi nimekamilisha, na kwa yale machache ambayo sikuyakamilisha, yatatekelezwa na uongozi ujao.
âRais Nyerere aliongoza kwa miaka 23 kuna mambo hakumaliza, Rais (Ali Hassan) Mwinyi amekaa madarakani miaka 10, (Benjamin) Mkapa miaka 10 hawakumaliza kila kitu. Ninaondoka madarakani nikiridhika kuwa mambo mengi nimekamilisha.
Katika mazungumzo ya viongozi hao, Kikwete alisema wamekubaliana namna ya kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kupendekeza maeneo mapya ya ushirikiano.
OP Habari Leo
Recent Comments