NA,ANKO G
Kufuatia ukosefu wa maji yanayotokana na mradi wa maji Kata ya Kabanga wialayani Ngara mkoani Kagera kwa kile kinacho daiwa kuwa ni hitirafu ya mtambo wa kupandisha maji imepekekea gharama ya maji kupanda.
Aidha wauza maji wamelazimika kupandisha bei ya maji kutokana na kutumia muda mwingi kuchota maji hasa katika vituo vya kuchotea maji vya watu bunafsi na taasisi kwasababu ya foleni ya wananchi wengi wanao chota maji katika vituo hivyo.
Vilevile wauza maji kwa kutumia usafiri wa Baiskeli na Pikipiki kwasasa wanalazimika kuuza Tsh 400 mpaka Tsh 500 kwa dumu lenye ujazo wa lita 20.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanalazimila kuchota maji ya kutoka kwenye mito na mabonde kwa kuogopa gharama na kuokoa muda wa kutafuta maji kwenye vituo binafsi.
Pia mvua inaponyesha inakua msaada mkubwa kwani wananchi hulazimika kukinga maji ya mvua ambayo huwasaidia katika matumizi yao.

Kwasasa maji yamekua changamoto Kabanga na tumaini la wananchi litarejea mpaka pale ambapo mamlaka husika itakapo karabati mtambo huo na huduma ya maji kurejea kwa wananchi.
