RAIS Jakaya Kikwete ameeleza kuridhishwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua iliyofikiwa ya kuweza kusajili jina la biashara kwa njia ya mtandao na kupata cheti ndani ya saa moja.
âHatua hii ya Brela ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,â alisema Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Pongezi za Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini, ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi.
Akithibitisha maendeleo hayo, mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Vibindo, alisema hivi karibuni alifanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu. Brela imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.
Mteja wa Brela anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
Anatakiwa kuingia katika mtandao wa Brela ambao ni www.brela. go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.
Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments