KILIMO CHA MIGOMBA KISICHO NA TIJA CHANZO CHA UMASIKINI NGARA.

By Simamia Ngara Apr 25, 2024

NA,ANKO G.

Asilimia kubwa ya wakazi wa Ngara wanamiliki aridhi lakini wengi wao hulima kilimo cha mazoea kisicho na tija ambacho hutoa mazao yasiyo faa kwenye soko.

Aidha simamia.com imefika Mabawe mukaliza na kushuhudia sehemu kubwa ya aridhi ikiwa na migomba ambayo hali yake hairidhishi kuzalisha ndizi zinazo faa kuuzwa sokoni.

Vilevile migomba hiyo inaonekana kuwa ni mbegu za kizamani ambazo hazikupandwa kitaalamu huku migomba hiyo ikiwa imesogeleana sana kiasi ambacho siyo rahisi kuwa na migomba mizuri.

Hata hivyo ndizi zinazo patikana kwenye migomba hiyo ni ndogo kiasi kwamba hazifai kuuzwa sokoni zaidi zinaliwa kwa matumizi ya nyumbani jambo linalo pelekea kushusha uchumi wa wakazi wengi wa Mabawe Mukaliza.

Pia ghalama ya mbegu na matunzo ya migomba yakisasa ni sababu ya wakulima wengi kuendelea kulima migomba ya kizamani ambayo mazao yake siyo mazuri.

Hivyo basi kuna haja ya serikilali kuweka mkakati mzuri wa kuhamasisha kilimo cha kisasa na maafisa kilimo kuwafikia wakulima na kufuatilia maendeleo ya mazao wanayo lima hasa migomba kama wanavyo fanya nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *