UVCCM KAGERA YATANGAZA KUPOTEZA WATU WANAO WATUKANA VIONGOZI

By Simamia Ngara Apr 24, 2024

NA,MWANDISHI WETU.

Mwenyekiti ya UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhani amesema kuwa wanao shinda mtandaoni na kuwatukana viongozi watawapoteza na jeshi la Polisi lisiwatafute ameyasema hayo katika ziara ya viongozi wa UVCCM wilayani Ngara.

“Kama kuna mtu anadhani anao uhuru wa kukaa mtandaoni na kisimu chake anashinda asubuhi kutwa nzima anatukana viongozi jeshi la Polisi hawa tukiwapoteza msiwatafute hawa piga makofi kwa CCM” Amesema Faris Buruhani Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kagera.

Aidha Buruhania ametumia ziara hiyo kikiasa chama cha mapinduzi kupiga chini wagombea wasio na sifa ili Chama Cha Mapundu kisitumie nguvu kubwa kufanya kampeni za kuwasafisha.

Vilevile Buruhani amesema kuwa mikopo ya 10% Kwa vijana inaenda kurejea mwezi July 2024 na kuwataka vijana kutengeneza vikundi vinavyo eleweka vyenye kuwa na sifa za kukopesheka.

Pia ameahidi kuzungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera Kikundi cha Kabanga Chalk kiweze kupata soko la kuuza Chaki zake katika shule za mkoa wa Kagera wakua wanazalisha chaki nzuri na zenye ubora wa hali ya juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *