WANNE WAFARIKI NGARA KWA AJALI YA MOTO

By Simamia Ngara Apr 26, 2024

NA, MWANDISHI WETU.

NGARA:Watu wanne wamefariki dunia na wengine saba wamenusurika kifo baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kushika moto usiku wa kuamkia Aprili25,2024 katika kijiji cha Rusumo waikaya ya Ngara mkoani Kagera.

Aisha kamanda wa Jeshi la zimamoto mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji, Zabrone Muhumha amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya Aprili 25 mwaka huu.

Vilevile amesema nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba vinne ilikuwa na watu 11 waliofariki walikuwa wamelala chumba kimoja ambacho kilikuwa na madumu ya petroli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *