VIONGOZI WA WILAYA YA NGARA WAOMBWA KUUTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA BARABARA KABANGA

By Mwafrika May 1, 2024

Na mwafrika

Hivi karibuni pametokea malalamiko kwa baadhi ya wananchi wa kata ya kabanga kuhusu kiwango cha ujengeji wa mfereji wa kupitisha maji taka katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha rami.

Hayo yametokea baada ya Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Mita zisizopungia 200 za kiwango cha Lami katika mitaa ya kimilamila inayopatikana kwenye kijiji cha kabanga wilani Ngara.

Baadhi ya wananchi wameonesha kupatwa na wasiwasi wa ujenzi wa Mfereji huo ambao kwa asilimia kadhaa umejengewa kwa udongo na cement huku wananchi has wakisema huenda mradi huo ukaharibika haraka kutokana na ujenzi unavyoendelea na kiwango kisichowaridhisha.

Hayo yote ni kwa mujibu wa baadhi ya wananchi wa kijiji cha kabanga ambao wamewaomba viongozi wa Wilaya kutembelea mradi huo ill kujiridhisha kwa macho yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *