KUPEKUA SIMU YA MWENZA WAKO NI KOSA LA JINAI

By Simamia Ngara Apr 26, 2024

NA, ANKO G.

Kwa mujibu wa Ibara ya 16 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema, “Kila Mtu anastahili kuheshimiwa na kupata Hifadhi kwa Nafsi yake, Maisha yake Binafsi na Familia yake na Unyumba wake, na pia Heshima na Hifadhi ya Maskani yake na Mawasiliano yake ya Binafsi”

Aidha licha ya katiba ya nchi kuweka wazi kuheshimu na kuto ingilia uhuru wa mawasiliano ya mtu binafsi imekua kawaida watu kuendelea kuvunja sheria hiyo kwa kupekua na kufuatilia mawasiliano ya wapenzi/wenza wao kitu ambacho ni kinyume na katiba ya nchi.

Hata hivyo tabia hiyo imekua chanzo cha kuharibu na kuvunja mahusiano mengi na hata kupelekea watu wengine kupata ulemavu wa kudumu na hata kupoteza maisha.

Pia kila mtanzania anapaswa kutambua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya nchi ya Tanzania na kufanya hivyo kunaweza kupelekea mtu kuchukuliwa hatua za kisheria pale anapo fanya hivyo.

Ifahamike kuwa mawasiliano ni faragha ya mtu binafsi na ndiyo maana nchi imeweka sheria ya kusajili laini za simu kwa kutumia taarifa binafsi na hata kujisajili kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia taarifa binafsi za mhusika anae tumia mawasiliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *