TAHADHARI KATIKA UJENZI WA LAMI KABANGA

By Simamia Ngara Apr 24, 2024

NA,ANKO G.

Kwa mara ya kwanza Kata ya Kabanga inaenda kupata barabara ya mtaa yenye kiwango cha lami yenye urefu wa Mita 200 ikiwa na umbo la herufi T.

Aidha barabara hiyo itaanzia kilipo kituo cha mabasi (Stand) na kuunganisha kipande cha Msikitini (soko kuu) mpaka ofisi ya CCM (Kimilamila).

Hata hivyo ujenzi huo unaendelea ambapo mpaka sasa hatua ya kumwaga kifusi imekamilika pamoja na kuweka mifereji ya kupitisha maji.

Hivyo basi kutokana na matumizi ya Barabara hiyo huna haja ya kuzingatia viwango vya ubora kwasababu endepo itajengwa chini ya kiwango kuna uwezekano wa kuharibika haraka kwasababu ni barabara inayo tumiwa na magari makubwa (Maroli) yanayo ingiza miziko soko kuu kila siku.

Hali kama hiyo umeshuhudiwa katika Soko la Buguruni Sokoni,Mabibo,Ilala na masoko mengine yanayo ingiza magari makubwa kupakia na kushusha mizigo barabara kuharibika kutokana na ubora wa barabara kuto endana na matumizi.

Kiwango cha barabara kilicho jengwa yalipo maegesho ya maroli Kastam Kabanga kingefaa sana ndicho kitumike lakini kama siyo mpango uliopo kunahaja ya kuweka kiwango cha lami cha kubeba zaidi ya tani 30.

Pia diwani wa kata hiyo Mh.Hafidh Abdallah amesha omba mita 400 zitakazo jengwa mwaka ujao 2025 ili kukamilisha mita 600 za kiwango cha lami.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *