VIJANA TUSIJISAHAU KWENYE UONGOZI

By Mwafrika Apr 18, 2024
Vijana - Tusisahau kushiriki kutafuta nafasi mbali mbali za uongozi. Hii ni serikali ya wote na hii ni nchi ya wote. Tusiogopeshwe na majigambo ya wanasiasa wenye nia ya kulinda nafasi walizomo kana kwamba wana hati miliki nazo. Vijana, huu ni muda wetu na tusiendelee kutulizwa na kudanganywa kuwa nafasi yetu ni kesho. Leo ndio nafasi yetu ya kuongoza na kujenga nchi yetu kwa manufaa ya jamii nzima.

Kwa miaka ya nyuma huko kulikua na maneno mengi kuhusu vijana kutopewa nafasi za uongozi jambo ambalo watu wengi ikiwemo vijana wenyewe wakiamini wao wanafaa kupewa nafasi za uongozi ama kuongoza.

Ila kwa sasa vijana wamepata nafasi ya kuongoza maana kuanzia ngazi ya chama tayari walishatoa nafasi ambazo hakuna atakaeziongoza ama kuzishika isipokua vijana wenyewe yaani kiufupi mbuzi kafia kwa muuza supu.

Kuna kauli ambayo inatembea mitandaoni ya miongoni mwa vijana waliosminiwa na kupewa dhamana ambapo yeye sasa baada ya kuoata nafasi anawaambia watu wakichagua uponzani basi hawatapewa maendeleo sasa swali la kujiuliza kwani nchi hii inaongozwa na upinzani?kuanzia lini?

Lakini pia kwanini kila siku ni vijana tu ambao ndio tunakoses au tubateleza au tuseme ndimi zetu hazina nifupa au ni kujisahah au tuseme ni basi tu mambo ya ubarobaro.

 

Vijana – Tusisahau kushiriki kutafuta nafasi mbali mbali za uongozi. Hii ni serikali ya wote na hii ni nchi ya wote. Tusiogopeshwe na majigambo ya wanasiasa wenye nia ya kulinda nafasi walizomo kana kwamba wana hati miliki nazo. Vijana, huu ni muda wetu na tusiendelee kutulizwa na kudanganywa kuwa nafasi yetu ni kesho. Leo ndio nafasi yetu ya kuongoza na kujenga nchi yetu kwa manufaa ya jamii nzima.

Ok ishu sio hiyo ishu hapa ni nini maana ya upinzani hasa kqenye siasa,je chama kinachoingoza nchi hakiwezi kuwa uoinzani kwa baadhi ya maeneo?vipi ikitokea chama fulani kikachukua jimbo ama kata na chama tawala kikakosa hapo tunahitaji hapo si mtawala kawa mpinzani?

Ok basi mimi kama simamia.com niwashauri tu vijana tuchunge kauli zetu maana hata nyimbo zina sema maneno yakishatoka hayarudi tena mdomoni na maji yakimwagika hayazoleki lakini pia tukumbuke mtoto akiunyea mkono haukatwi yaani unaoshwa alafu mambo yanaendelea.