JUMUIYA YA ASKARI WAISLAMU MKOA WA MOROGORO WATOA MKONO WA IDI KWA WAFUNGWA.

By Mussa Mathias Apr 10, 2024

JUMUIYA YA ASKARI WAISLAMU MKOA WA MOROGORO WATOA MKONO WA IDI KWA WAFUNGWA.

Na Musa Mathias, Morogoro. 

Email. mussamathias573@gmail.com

Jumuiya ya Askari (dini ya) Waislamu wa Mkoa wa Morogoro wametoa mkono wa Idi (mahitaji ya Sikukuu) kwa wafungwa na Mahabusu wa gereza la Morogoro mjini ikiwa ni sehemu ya kuwashika mkono ili wajisikie vyema kushiriki sikukuu hii kwa kula na kunywa pamoja nao.

Akiongea na Mahabusu hao Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) Yohana Mjengi ambaye amemuwakilisha Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro amesema, wamefikia hatua hiyo baada ya kusikia kuna wafungwa na Mahabusu mbalimbali kuwa watu hao wapo gerezani lakini wameshiriki kwenye ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha amewataka wawe wasikivu na wabadilike kimatendo na kufuata sheria na taratibu za nchi mara baada ya kutoka gerezani.

Naye Mkuu wa gereza la Mahabusu mkoa wa Morogoro SP Nicodemus Tenga amewashukuru Askari hao na kuwaomba Wananchi na taasisi nyingine kuiga mfano wa Polisi Morogoro kwa kuwasaidia na kuwakumbuka makundi ya watu wenye uhitaji kwani huwafanya kujihisi nao ni wanajamii.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Badru Mtambo muwakilishi wa Jumuiya ya Polisi Waislamu Mkoani hapo amesema, pamoja na yote yaliyotokea kuwahusu wafungwa na mahabusu, bado ni ndugu zetu na wanapaswa kusheherekea Sikukuu kama watu wengine hivyo kulikuwa na umuhimu wa wa kuwapelekea mahitaji hayo.