WANAWAKE MIKUMI WALIVYOULA KUPITIA MRADI WA REGROW

By Mussa Mathias Apr 18, 2024

WANAWAKE MIKUMI WALIVYOULA KUPITIA MRADI WA REGROW.

 

Na Musa Mathias.

 

Email. Mussamathias573@gmail.com

 

Kilosa – Morogoro.

 

VIKUNDI vya wanawake Kata ya Msongozi wilayani Kilosa mkoani Morogoro vinavyojihusisha na shughuli za ujasiriamali kupitia Benki za Hifadhi za Jamii COCOBA wameeleza shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwainua kiuchumi kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).

 

Kabla ya mradi huo, wanawake wengi walikabiliwa na umaskini na walitegemea shughuli haramu za ujangili kama njia mbadala ya kujipatia kipato. Pamoja na kuhatarisha maiosha yao shughuli hizo zilikuwa chanzo cha umaskini wao kuendelea.

 

Kaimu Afisa Mtendaji wa Mikumi, Method Msimbe amesema kupitia Mradi wa REGROW, wanawake wa kijiji cha Mkata kilichopo kata ya Msongozi wilayani Kilosa wamefanikiwa kubadili maisha yao.

 

Alisema kuwa mradi huo umeleta mabadiliko makubwa kwa vikundi 15 vyenye jumla ya wanachama 327, wakiwemo wanawake 265.

“Wanawake hawa wameweza kuanzisha biashara mbalimbali na kuboresha maisha yao kwa kiasi kikubwa” alisema Msimbe.

 

Nadya Hassan ni mmoja wa wanawake walionufaika na mradi wa REGROW anaeleza kuwa amejikomboa kutoka umaskini kwa kumiliki biashara mbalimbali ikiwemo duka la dawa na mashamba ya miwa.

MOJA YA MRADI AMBAO WANAUTEKELEZA KUPITIA UWEZESHWAJI KUTOKA REGROW. 

 

“Kabla ya mradi huu nilikuwa na duka dogo la dawa lenye faida ndogo. Lakini baada ya kujiunga na mradi wa REGROW, niliweza kupata mtaji wa kuongeza dukani na pia kununua mashamba ya miwa. Sasa anapata faida kubwa zaidi na naweza kuboresha maisha yangu na familia yangu” alisema Nadya.

Aidha kikundi cha Tupendane chekereni kilichoanzishwa Mei 14, 2022 baada ya wanawake 21 kuamua kukianzisha kufuatia mafunzo ya cocoba yaliyotolewana mradi kimepiga hatua kubwa kiuchumi.
Wanawake hao walioanza na mtaji wa Sh 111,000 walipatiwa mtaji mbegu wa sh 11,134,800 na kukopeshana.
Wakati kikundi kilipoanza walikuwa wanakopeshena Sh laki mbili kwa sasa wanakopeshena zaidi ya Sh milioni 3 kutoklana na mtaji kuongezeka kufikia milioni 26/

Aidha kikundi hicho kinamiliki mradi wa kukamua mafuta ya alizeti uliofadhiliwa kwa sh milioni 28.8

 

 

 

Mradi wa REGROW unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ukiuwa umelenga kuboresha usimamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa na kukuza utalii kusini mwa Tanzania.

Mradi unatarajiwa kunufaisha watu zaidi ya 100,000 katika mikoa ya Morogoro, Lindi na Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo hadi sasa wanawake zaidi ya 9,386 wamewezeshwa kiuchumi kupitia mradi wa REGROW.
Kutokana na kuongezeka kwa shughuli za ujasiliamali kwa wakinamama mapato ya Halmashauri ya Mji wa Mikumi pia yanaendelea kukua.

Wanawake wa hao wa Mikumi wametoa shukrani za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Mradi wa REGROW na kusema mradi huo umebadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na umewawezesha kuwa wanawake wajasiliamali wenye mafanikio.

Mwisho.