ZIARA YA MKUU WA MKOA WA KAGERA MH HAJAT FATMA ABUBAKAR MWASSA YALETA FURAHA WILAYANI NGARA KATA YA KABANGA

By Mwafrika Jul 27, 2023

Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Hajat Fatma Abubakar Mwassa wilayani Ngara imezaa matunda baada ya kutatua kero ya eneo la kuegeshea magari lilohamishwa kutoka sehemu ya kwanza ambapo wananchi walikua wakipata faida kwa kufanya biashara kutokana na malori kujaa kwa wingi.

Hayo yamefanyika baada ya diwani wa kata ya kabanga mh Hafidh Abdalah kuomba Mkuu wa mkoa kutatua tatizo hilo ambalo ni kero ya muda mrefu kwa watumiaji wa eneo hilo ikiwepo madereva kukosa huduma ya Internet (mtandao kuwa chini)hivyo kukosa mawasiliano mazuri.

Baada ya kusikiliza mkuu wa mkoa Mh Hajat Fatma Abubakar Mwassa Aliomba kupelekwa kuona maeneo hayo yaani parking ya zamani na sasa kisha baada ya kujionea akatatua kero hiyo kwa kutoa maelekezo kuanzia tarehe 26/7/2023 kuhamishwa na kurudishwa ilipokua mwanzo.

Haya ni miongoni mwa matunda ya ziara hiyo pamoja na kuwaomba watu wa uhamiaji na Nida kuangalia namna nzuri itasaidia wananchi wa Ngara wanapata huduma ya Vitambulisho vya uraia(namba)kwa utaratibu mzuri.

 

One thought on “ZIARA YA MKUU WA MKOA WA KAGERA MH HAJAT FATMA ABUBAKAR MWASSA YALETA FURAHA WILAYANI NGARA KATA YA KABANGA”
  1. Simamia, mnahatarisha amani ya kiongozi wenu. Pelekeni mambo taratibu ama sivyo ataendelea kuombewa na wachungaji mbali mbali kwani wanamuona kama anahitaji neema za Mungu tuu. Wanangara, na si Mungu, ndio wapiga kura, sasa hata mapepo yote yangemtoka , ataendelea kulazimisha umma upended. Mbona mazuri ya viongozi wengine yanajiongelea na wao hawasisitizi na kulazimisha upend. Huyu kakosea wapi ama ameshindwa kusimamia lipi?

    Akakandike tuu.

Comments are closed.